WAANDAMANA KUPINGA MICHEZO YA KOMBE LA MABARA


Brazilian police block protesters from entering Maracana soccer stadium in Rio on June 16, 2013.
Polisi wa Brazili wakiwazuia waandamanaji kuingia katika uwanja wa soka wa Maraca mjini Rio tarehe 16 Juni 2013.



Polisi nchini Brazili wametumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kuutawanya umati wa watu wapatao 3,000 waliokuwa wakiandamana nje ya uwanja wa Soka wa Maracana mjini Rio de Janeiro kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kombe la Mabara.


Maandamano hayo yalifanyika jana Jumapili kupinga kiwango kikubwa cha fedha za umma kilichotumika kuandaa mashindano hayo.


Aidha, waandamanaji hao walipinga kiasi kikubwa cha gharama za maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka ujao, kiwango kinachotarajiwa kufikia Dola bilioni 15.



“Sijali kuhusu Kombe la Dunia- Ninataka afya na elimu!" walipiga kelele waandamanaji hao.



Awali, polisi walijipanga katika msitari na kuweka kizuizi nje ya uwanja huo wa soka kuwazuia waandamanaji hao. Hata hivyo, umati wa waandamaji ulijaribu kuvuka kizuizi hicho bila mafanikio. 



Mnamo Juni 15, polisi walikabiliana na maandamano mengine kama hayo wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Mabara katika mji mkuu, Brasilia.



Makabiliano hayo yalihitimishwa kwa watu 39 kujeruhiwa baada ya polisi kutumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kuutawanya umati wa waandamanaji.


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment