UINGEREZA KUWALIPA FIDIA WANAMAPAMBANO WA MAU MAU



Uingereza imekubali kulipa shilingi bilioni 1.8 za Kenya kwa ajili ya kuwafidia maelfu ya Wakenya walioteswa wakati wa mapambano ya Mau Mau dhidi ya wakoloni hao wakongwe wa Ulaya.

William Hague, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anatarajiwa kutangaza malipo ya Shilingi bilioni 1.8 kwa waathirika 5,000 wa mateso yaliyofanywa na wakoloni wa Uingereza katika miaka ya 50 malipo ambayo yatakuwa ni sawa na Shilingi 340,000 za Kenya kwa kila mtu mmoja.

Waathirika wa tukio hilo wanasema kwamba walitendewa vitendo vibaya mno na wakoloni wa Uingereza ikiwa ni pamoja na kubakwa, kupigwa na kuhasiwa wakati walipokuwa wamekamatwa na vikosi vya Uingereza na vibaraka wao kwenye mapambano hayo.

Uingereza imeamua kutoa fidia hiyo baada ya wiki kadhaa za mazungumzo yaliyowashirikisha wanasheria pamoja na wawakilishi wa waathirika hao ambao walitishia kuwa iwapo hawatofidiwa basi wangeliishitaki serikali ya London.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment