JE, AKINA MUSEVENI WANAJITENGA?



Hapo jana Marais Museveni, Kagame na Kenyatta walikutana nchini Uganda. Baadhi ya watu wamekuwa wakihoji juu ya mkutano huo ambao, pamoja na mambo mengine, ulijadilia masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki bila uwepo wa Marais wenzao wa Tanzania na Burundi. Hapa chini tumeweka kwa mukhtasari baadhi ya mambo yaliyojadiliwa na viongozi hao.

Mkutano wa jana baina ya marais wa Uganda, Kenya na Rwanda uliofanyika katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda uliazimia mambo yafuatayo:

1.    Kuondosha mizani na vizuizi vya barabarani ili kurahisha biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.

2.    Uondoshaji wa mizigo kufanyika mara moja kutoka Mombasa.

3.    Pia walikubaliana kuwa na kadi za vitambulisho na viza moja ya utalii.

4.    Kuoanisha shughuli za kodi.

5.    Kujenga bomba la pili la mafuta.

6.    Kamati ya ufuatiliaji kukutana kila baada ya wiki mbili kutathmini maendeleo.

7.    Kugawana majukumu ili kufikia malengo hayo. Uganda itasimamia na kuongoza suala la reli, usafishaji wa mafuta na shirikisho la kisiasa. Kenya itasimamia suala la uzalishaji na ugavi wa umeme na ujenzi wa mabomba ya mafuta, huku Rwanda ikisimamia suala la ushuru wa forodha, viza ya moja ya utalii na vitambulisho vya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

8.    Licha ya kutokuwepo kwa viongozi wengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Marais Museveni, Kagame na Kenyatta katika kikao hicho pia walikubaliana kuharakisha uundwaji wa Shirikisho la Afrika Mashariki. Walieleza kuwa kumekuwepo na hali ya kusuasua katika uundwaji wa Shirikisho hilo la kisiasa na hivyo kuna haja ya kuharakisha mchakato na kuhakikisha linakamilika.


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment