![]() |
| Wabunge wa Taiwani wakichapana makonde bungeni Jumanne Juni 25, 2013. |
Rabsha ilizuka katika bunge la Taiwan kati ya vyama vikuu vya siasa juu ya muswada wenye utata.
Jana Jumanne, wabunge wa chama tawala cha Kuomintang waliripotiwa kushikilia kipaza sauti katika hatua iliyolenga kukizuia chama cha upinzani, Democratic Progressive Party (DPP) kisipinge muswada wa kodi ya mitaji.
Muswada huo wenye utata ulipitishwa mwaka jana na chama tawala na kuanza kufanya kazi mwezi Januari mwaka huu. Lakini, muswada huo umekuwa ukipingwa vikali na wafanya biashara na makampuni mbalimbali. Katika rabsha hizo, Wabunge kadhaa waliripotiwa kujeruhiwa.
Wakati huo huo, mwanaharakati maarufu wa China mwenye ulemavu wa macho, Chen Guangchen, alipoitembelea Taiwan alisema kuwa "ni bora kuona rabsha bungeni kuliko kuona vifaru vikipita mitaani na kwenye viwanja mbalimbali.”
Mwishowe chama tawala kilipitisha mapitio yake ya muswada wa kodi ya mitaji.
Serikali ya Taiwan inasema kuwa muswada huo ni wa muhimu ili kuondosha pengo baina ya masikini na matajiri.
visiwa vya Taiwan na eneo la bara la China zimekuwa zikiongozwa tofauti tangu ulipotokea mpasuko mwaka 1949 mwishoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe lakini China inaviona visiwa hivyo kuwa ni sehemu ya eneo lake linalosubiri kuunganishwa.

0 comments:
Post a Comment