ISRAELI YAISHAMBULIA GAZA

An Israeli air raid on the Gaza Strip in November 2012 (file photo)
Mashambulizi ya Ndege za Israeli dhidi ya Ukanda wa Gaza mwezi Novemba 2012.




Ndege za kivita za Israeli zimefanya mashambulizi ya anga katika maeneo ya kati na kusini mwa Ukanda wa Gaza, lakini mpaka sasa hakuna ripoti za majeruhi na maafa kutokana na mashambulizi hayo.


Mashambulizi hayo dhidi ya eneo hilo lililowekewa mzingiro yametokea alfajiri ya leo katika kile ambacho Israeli inasema kuwa ni kujibu mapigo ya makombora yaliyorushwa kutoka Gaza.


Ripoti za vyombo vya habari zinasema kuwa Israeli ilishambulia maeneo matatu katika Ukanda huo unaotawaliwa na vuguvugu la harakati ya Hamas.


Mashuhuda wa Kipalestina wanasema kuwa mashambulizi hayo yalipiga katika maeneo yasiyokuwa na makazi na hivyo hakuna majeruhi au maafa yaliyoripotiwa.



Wakati huo huo, maafisi wa Israeli, wamekilaumu kikundi cha Islamic Jihad cha Palestina kwa "angalau makombora sita" yanayodaiwa kurushwa kutoka eneo la kaskazini mwa Gaza.



Aidha, watawala wa Israeli walisema kuwa makombora hayo hayakusababisha hasara au majeruhi wowote.


Siku ya Jupili, vyombo vya habari vya Israeli viliripoti kuwa ving'ora vilisikika katika maeneo kadhaa ya kusini mwa Israeli na makombora mawili yalinaswa na mitambo maalumu ya kuzuia makombora ya Iron Dome katika eneo la Ashkelon.


Aidha, msemaji wa jeshi la Israeli alidai kuwa ndege za Israeli ziliyalenga "maeneo yalikotoka makombora husika."


Mnamo Mei 13, On May 13, shambulizi la Israeli liliyalenga maeneo ya mji wa Beit Hanoun kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.


Katika miezi ya hivi karibuni, Israeli imefanya mashambulizi kadhaa katika Ukanda wa Gaza ikiwemo shambulizi la mwezi Mei katika mji wa Beit Hanoun na mashambulizi matatu ya anga mapema mwezi Aprili katika mji wa kusini wa Khan Younis na jirani na mji wa Rafah. 



Mwezi Novemba 2012, vikosi vya jeshi la Israeli vilianzisha operesheni maalumu waliyoiita Operesheni ya Nguzo ya Ulinzi I dhidi Ukanda wa Gaza. Zaidi ya Wapalestina 160, wakiwemo wanawake na watoto, waliuawa na wengine wapatao 1,200 kujeruhiwa katika vita hiyo ya siku nane.


Katika kujibu, wapiganaji wa Kipalestina walirusha makombora kuelekea upande wa Israeli na kuwaua watu 5. Hujuma hizo zilikoma baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosainiwa na Hamas na Israeli kwa usimamizi wa Misri.


Kwa mujibu wa msemaji wa Hamas, hujuma hizo za Israeli dhidi ya Ukanda wa Gaza zilisababisha hasara yenye thamani ya Dola bilioni 1.2.


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment