WIMBI JIPYA LA MAANDAMANO LAITESA BRAZIL

Brazilians hold an anti-government protest along Rio de Janeiro’s Copacabana beach on June 23, 2013.
Wabrazil wakiandamana kwenye ufukwe wa Copacabana mjini Rio de Janeiro Juni 23, 2013.



Wananchi wa Brazil wamefanya maandamano mapya nchini kote katika hali ambayo  wananchi wengi wameendelea kuwaunga mkono waandamanaji wanaotaka mabadiliko ya kiserikali na huduma bora za jamii.


Siku ya Jumapili, maandamano yalihanikiza katika miji kadhaa, ikiwa ni pamoja na watu 4,000 kuandamana katika fukwe maarufu ya Copacabana mjini Rio de Janeiro na katika mji wa kaskazini mashariki wa Fortaleza, ambapo mchezo wa mwisho wa Kombe la Mabara ulikuwa ukichezwa.  

Watu wamekuwa wakimininika mitaani kwa muda wa wiki mbili kuonesha hasira zao dhidi ya ubadhirifu na ufisadi mkubwa wa serikali na gharama kubwa ya kuandaa mashindano ya Kombe la Dunia la mwaka 2014.



“Tunapenda soka, unajua kuwa sisi ni Wabrazil. Lakini hiyo haina maana kwamba tunataka kumwaga mabilioni ya pesa. Tunatoa kiwango kikubwa sana cha kodi, gharama za ujenzi wa viwanja vipya vya soka ni za juu sana," alisema mmoja wa waandamanaji.


Brazil itatumia dola bilioni 26 katika pesa za umma kwa ajili ya Kombe la Dunia. Baadhi ya waandamanaji pia waliilaumu FIFA na kusema kuwa ndiyo inayopanga masuala yote ya uwekezaji katika tukio hilo.


Maandamano ya siku mbili zilizopita yanaonesha kuwa waandamanaji wengi hawakuridhishwa na ahadi zilizotolewa na Rais wa Brazil Dilma Rousseff Juni 21 za kuboresha huduma za umma na kuzidisha mapambano dhidi ya ufisadi uliokithiri katika nchi hiyo.


Uchunguzi wa maoni uliotolewa Juni 22 na shirika la Ibope ulionesha kuwa robo tatu ya Wabrazil wanayaunga mkono maandamano hayo.


Maandamano yalizuka Juni 11, baada ya wananchi katika mji wa Sao Paulo kuingia barabarani kulaani ongezeko kubwa la nauli katika usafiri wa umma.


Machafuko yalisambaa haraka nchini kote na mpaka Juni 22 kiasi cha watu 1.5 walishiriki katika maandamano.


Katika baadhi ya maeneo, polisi waliamua kutumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji.


Waandaaji wa maandamano wameapa kuendelea na maandamano mpaka zitakapochukuliwa hatua za msingi kubadilisha mfumo wa kisiasa wakati ambapo vyombo vya habari vimeitisha mgomo mkubwa  mnamo Julai 1, wakisema, “Julai 1, 2013, Brazil itasimama.” 
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment