Mbeya. Wanafunzi 15, wa Shule ya Sekondari ya Jumuiya ya Wazazi ya Lupata wilayani Rungwe mkoani Mbeya , wanashikiliwa polisi kwa tuhuma za kuchoma moto bweni la wanafunzi wa kiume na kusababisha uharibifu wa mali mbalimbali.
Aizungumzia tukio hilo , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 2:00 usiku shuleni hapo na kwamba wanafunzi hao walifikia hatua hiyo ya kuchoma moto bweni hilo, wakipinga kusimamishwa masomo kwa wanafunzi wenzao watatu kwa utovu wa nidhamu.
Aliwataja wanafunzi waliosimamishwa masomo kwa utovu wa nidhamu kuwa ni Joseph Robert (18), anayesoma kidato cha nne na Mwita Chacha (17) na anayesoma kidato cha tatu, wote wakazi wa Kitunda jijini Dar es Salaam na Mwingine ni Daniel David (18), anayesoma kidato cha tatu ambaye ni mkazi wa Ipinda wilayani Kyela.
Alisema kuwa wanafunzi hao watatu waliwahamasisha wenzao kuwaunga mkono kupinga adhabu hiyo kwa kufanya vurugu na kwamba bweni lililochomwa moto walikuwa wanaishi wanafunzi 50, ambao hawakuwa tayari kuunga mkono uvunjifu huo wa amani.
CHANZO:MWANANCHI
CHANZO:MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment