Rais Wa Marekani Barack Obama Anatarajiwa Kutembea Tanzania Mwezi Ujao


Rais Barack Obama wa Marekani anatarajia kuanza ziara yake ya pili katika bara la Afrika mwishoni wa mwezi June, ziara ambayo itamfikisha Africa ya Kusini, Tanzania na Rwanda.
Katika ziara yake hiyo, atapitia Nigeria na kuongea na rais Goodluck Jonathan pamoja na waandamizi wa serikali ya Nigeria.
 Mpango wa awali ulikuwa kwamba rais Obama angetembelea Nigeria kwa siku mbili lakini kutokana na hofu ya usalama kutoka kw Boko Haram Wa Nigeria inaonekana kwamba itashindwa kutoa ulinzi wa kutosha wa rais huyo wa Marekani hivyo atalazimika kukaa Nigeria kwa muda mchache.
Habari kutoka Ikului ya White House zinadokeza kuwa usalama utazingatiwa sana katika ziara hiyo na kama kutakuwa na sababu yeyote ya kuwa na wasiwasi juu ya usalama wa Rais Obama basi ziara hiyo itakatizwa wakati wowote katika nchi ya Nigeria.
Mwaka 2009 Obama alitembelea Africa na alichagua nchi ya Ghana ambapo alikutana na Raisi (marehemu) John Atta mills, na akatoa hotuba katiba bunge la Ghana na kisha kutembelea Cape Coast Castle sehemu ambapo watumwa wa Trans Atlantic walikuwa wanapakiliwa kupelekwa Marekani wakati wa biashara ya utumwa.
Kwa sis watanzania, ziara hii ya kiongozi mkubwa duniani ina manufaa gani kibiashara, kiuchumi, kiusalama? Kuna fursa gani kwa Watanzania kama ilivyoluwa kwa Rais wa China? Ni matumaini yetu kuwa ziara hii itazidi kuliweka Taifa letu katika sura nzuri kimataifa na kitaifa. Ikumbukwe kwamba, Marais wa nchi kubwa kama Marekani wanachagua kutembelea nchi zile zinazofanya vizuri katika utawala bora, demokrasia madhubuti, uhuru wa haki za binadamu, uhuru wa vyombo vya habari, kusimamia na kutimiza vyema malengo ya millenium..... Hivyo kwa Tanzania kupata ugeni kama huu ni ishara nzuri na chachu ya kuendelea kufanya vizuri zaidi. Mungu Ibariki Tanzania
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment