PROF LIPUMBA AZINDUA KAMPENI YA UCHAGUZI MDOGO CHAMBANI

Na Bakar Mussa, Pemba

Wananchi wa jimbo la Chambani wameombwa kumchagua mgombea wa chama cha wananchi CUF, Yussuf Salim Hussein ili kuendeleza yale yaliochwa naaliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo marehemu Salum Hemed Khamis,katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Juni 16 mwaka huu. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Taifa, Profesa Ibrahim Haroun Lipumba aliyasema hayo wakati akiwahutubia wanachama wa chama cha CUF na wananchi wa Jimbo la hilo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo hilo.

Profesa Lipumba, alisema hayo katika kijiji cha Jongomeo jimbo la Chambani Wilaya ya Mkoani ukiwa ni mkutano wa kwanza wa chama hicho wa kumdani mgombe wa Chama hicho katika uchaguzi huo unaowashirikisha wagombea wanne kutoka katika vyama vine tofauti.

Mwenyekiti huyo aliwataka wananchi wote wenye shahada za kupigia kura kutopuuza kujitokeza siku ya uchaguzi kwa kumpigia kura mgombea wa chama hicho ili jimbo hilo liendelee kubakia katika mikono ya CUF.

Alisema kuwa CUF ndiyo chama chenye sera za kutaka kuleta mabadiliko ya kweli kwa wananchi wa jimbo hilo,Zanzibar na Tanzania kwa jumla, hivyo Wananchi wanayokila sababu ya kukichaguwa.

Alifahamisha kuwa ushindi wa mgombea huyo itakuwa ni kipimo tosha kwa chama hicho katika harakati za kushinda uchaguzi Mkuu wa unaokuja iwapo kitapata ridhaa ya kuongoza dola.

” Chama cha CUF kinaendelea kujipanga katika kuhakikisha uchaguzi mkuu wa 2015 chama hicho kinaingia Ikulu ili kiweze kutekeleza sera zake kwa vile hivi sasa kimo katika serikali ya umoja wa kitaifa lakini sera zinazotekelezwa ni za Chama cha Mapinduzi CCM, kwa vile ndio kinacho ongoza nchi” alisema Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Habari,Haki za Binadamu na Mawasiliano ya Umma, Salim Bimani, aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kusimamia uchaguzi huo katika misingi ya haki na uhuru, huku akivitaka vyombo vya Dola kusimamia Kampeni na uchaguzi kwa amani na utulivu.

“Naamini kuwa Tume ya Taifa ya uchaguzi itaendesha zoezi la uchaguzi huu kwa uadilifu na kupatikana mshindi atakayetokana na matakwa ya wapiga kura wa Chambani” na sio vyenginevyo.

Alifahamisha kuwa kwa upande wa chama cha CUF kitawahamasisha wananchi kujitokeza na mapema katika zoezi hilo na hatimaye itakapotimia saa kumi za jioni wananchi wote wawe wameshamaliza kupiga kura, ili kura zihisabiwe na ikifika saa kumi na mbili matokeo yatakuwa yameshatangazwa.

Wagombea wanaoshiriki katika uchaguzi huo mdogo ni Yussuf Salim Hussein- CUF,Mattar Sarahan Said-CCM, Said Miraji Abdalla -ADC na Siti Ussi Shaib wa CHADEMA ikiwa ni mwanamke pekee baada mwenzake Asha Muhsin wa NCCR-Mageuzi kushindwa kurejesha fomu.

Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chambani Pemba, unatarajiwa kufanyika tarehe 16 Juni, kuziba nafasi iliyowazi baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo (CUF), Salum Hemed Khamis kilichotokea Machi mwaka huu.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment