CUF YALAANI MAGAZETI KUENEZA CHUKI ZA KIDINI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

CUF TUNALAANI BAADHI YA MAGAZETI KUENEZA UCHOCHEZI WA KIDINI

Imetolewa na Abdul Kambaya
Naibu Mkurugenzi Habari, Uenezi na Haki za Binadamu
Mei 26, 2013

CUF – Chama cha Wananchi tumesikitishwa na baadhi ya magazeti (hususani Tanzania Daima) kuchochea hasama za kidini, na kuwabagua wananchi kwa mujibu wa imani zao huku wakihusisha chochezi hizo na baadhi ya Vyama vya kisiasa na viongozi wao, katika toleo Namba 3096 la Jumapili, Mei 26, 2013.
Kwa mujibu wa waandishi wa gazeti hilo George Maziku na Josephat Isango, ambalo linanalochapishwa kila siku na linamililokiwa na kampuni ya Freemedia ambapo umiliki wake unahusishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA) Freeman Mboe, muhusika mkuu aliehusishwa na tuhuma hizo za udini ni Prof. Ibrahim Haruna Lipumba Mwenyekiti wa CUF – Chama cha Wananchi.
Gazeti hilo pamoja na mambo mengi waliyoandika ambapo undani wake na tafsiri ni kutaka kuwaonyesha wananchi kuwa Prof. Ibrahim Lipumba na Dk. Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa ni wenyeviti wa vyama vyao na walikokuwa wagombea urais mwaka 2010 waligubikwa na imani za udini na waliendesha kampeni zao kwa kutegemea kura za waislam, na Prof. Lipumba amekuwa akitumia misikiti na viongozi wa dini hiyo ili waislam nchini waandelee kukiunga mkono chama chake, na hasa katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015.
Katika kuonyesha kuwa gazeti hili la Tanzania Daima limekusudia kuvigawa vyama vya siasa kwa falsafa ya udini, ni pale mwandishi anapomshutumua Rais Kikwete kwamba mwaka 2010 pamoja mgombea huyo wa CCM kuwashiwishi viongozi wa dini ya Kiislam kuwakataza waumini wao wasimuunge mkono mgombea wa CHADEMA ambae alishawahi kuwa Padre Dk. Silaa na ametumwa na Kanisa Katoliki lakini pia Propaganda hizo za Rais Kikwete alizielekeza kwa viongozi wa CUF na wafuasi wao kumpigia kura Muislam mwenzao yeye Kikwete huku wakiahidiwa kuwa Waislam wa CCM watampigia mgombea CUF mwaka 2015 kwa hoja kuwa CCM watakuwa wamesimamisha mgombea mkiristo. 
CUF – Chama cha Wananchi hatushangazwi na gazeti hili ambalo uandishi wake linatumikia utashi wa mmiliki wake, ambapo mwaka huu wameibuka wakiwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumuhusisha Rais Jakaya Kikwete na tuhuma za udini, hususani uislam, na hivyo wanataka pia tuhuma kama hizo wamuhusishe nazo Mwenyekiti wetu Prof. Ibrahim Haruna Lipumba.
CUF – Tunatambua kuwa Mwenyekiti wetu Prof. Ibrahim Haruna Lipumba ni Muislam, chama hakitoweza kumzuia kuhudhuria ibada katika msikiti wowote atakaotaka kwenda kuabudu na hata kualikwa iwe msikitini, kanisani na hata kwenye mahekalu ya kihindu na kutakiwa kutoa hutoba kwa waumuni wenzie au waliomualika, kama wafanyavyo viongozi wengine wa vyama vya siasa vikiwemo CHADEMA, CCM na vyama vingine, ambapo kumbukumbu zinaonyesha kuwa Rais wa awamu ya nne Benjamin William Mkapa alipokuwa madarakani alitangaza kuwapa Waislam chuo cha Tanesco Morogoro na kuwa Chuo Kikuu cha Kiislam na kutoka kauli kama ya Prof. Ibrahim Lipumba ya kuwataka “Waislam Wajipange” kwenye ibada aliyoalikwa na Waislam.
CUF – Tunasisitiza tunalaani gazeti hili la Tanzania Daima na tutaendelea kulaani chombo chochote kinachotaka kuwagawa Watanzania wawe ni Viongozi au wananchi kwa misingi ya dini zao, na tunaitaka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kutovifumbia macho vyombo ambavyo vinataka kutupeleka kusiko na hasa ukizingatia nchi yetu kwa sasa umegubikwa na matukio mengi yahusuyo migongano katika dini zetu na uharibifu wa nyumba za ibada. 

Kwa mawasiliano zaidi 0719 566567
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment