MLIPUKO WAUA WATU 14 NCHINI AFGHANISTAN



The site of a bomb attack in Afghanistan’s western province of Herat (file photo)
Mojawapo ya matukio ya milipuko ya mabomu katika jimbo la magharibi la Herat nchini Afghanistan. 



WATU kadhaa, akiwemo afisa mwandamizi wa serikali, wamepoteza maisha kufuatia mlipuko wa bomu katika jimbo la kaskazini mashariki la Baghlan, nchini Afghanistan.


Shambulio hilo la bomu lilitokea mbele ya jengo la baraza la jimbo katika mji wa  Pul-e-Khumri Jumatatu ya leo. Watu kumi na nne walipoteza maisha yao katika mlipuko huo.


naibu mkuu wa polisi wa jimbo hilo, Sadeq Muradi, alisema kuwa mkuu wa baraza la jimbo, Rasoul Mohseni, na walinzi wake ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha. Muradi aliongeza kusema kuwa watu 8 walijeruhiwa.


hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulio hilo.


mamlaka za Afghanistan zimeanzisha uchunguzi wa mlipuko huo.


Kwa miaka kadhaa sasa, maelfu ya watu wamekuwa wakipoteza maisha katika mashambulizi yanayotekelezwa na wapiganaji wa kundi la waasi wa Taliban na vikosi vya kigeni vinavyoongozwa na Marekani nchini Afghanistan.


Ghasia zimeendelea kuitikisa nchi hiyo licha ya kuwepo kwa maelfu ya askari ya kigeni kwa zaidi ya muongo mmoja baada ya uingiliaji kati ulioongozwa na Marekani mwaka 2001.


Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa mwezi Februari, zaidi ya watu 2,750 walipoteza maisha na wengine zaidi ya 4,800 kujeruhiwa katika mashambulizi mbalimbali mwaka uliopita. 
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment