IRAQ: ZAIDI YA WATU 30 WAPOTEZA MAISHA KATIKA MILIPUKO YA MABOMU



An Iraqi policeman stands at the site of a car bomb attack in Baghdad. (File photo)
Polisi wa Iraq akiwa amesimama kwenye eneo lililokumbwa na mlipuko wa bomu mjini Baghdad. 




Zaidi ya watu 30 wamepoteza maisha yao katika mfululizo wa milipuko ya mabomu ya kutegwa kwenye magari katika mji mkuu wa Iraq na mji wa kusini wa Basra.



Vyanzo vya usalama na hospitali nchini Iraqi vimesema kuwa milipuko hiyo ya mabomu ilitokea katika wilaya zinazokaliwa sana na wafuasi wa madhehebu ya Kishia mjini Baghdad leo Jumatatu. Kwa uchache watu 20 walifariki katika mashambulizi hayo.


Hakuna kundi lililodai kuhusika na milipuko hiyo, ingawa kumekuwepo na madai kuwa mashambulizi hayo yamekuwa yakifanywa na waasi wenye uhusiano na mtandao wa al-Qaeda wanaodaiwa kutaka kuiyumbisha serikali kuu.



Mapema leo, watu kumi na moja walifariki dunia baada ya milipuko miwili ya mabomu kuutikisa mji wa Basra, takriban kilometa 420 (maili 260) kusini mashariki mwa Baghdad.


Mlipuko wa kwanza ulitokea katika eneo la Hananiya karibu na eneo la soko lenye shughuli nyingi. Bomu la pili lilitokea ndani ya kituo cha basi katika Maidani ya Saad.


Tarehe 2 mwezi wa Mei, Tume ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Iraq (UNAMI) ilisema kuwa mwezi wa Aprili ndio uliokuwa mwezi mbaya kabisa nchini humo tangu mwaka 2008 baada ya watu 700 kuuawa na  wengine 1600 kujeruhiwa nchini kote.


Aidha, UNAMI ilisema kuwa jimbo la Baghdad ndilo jimbo lililoathiriwa zaidi baada ya watu 211 kuuawa na wengine wapatao 500 kujeruhiwa.


Jana Jumapili, polisi kumi walipoteza maisha baada ya watu wenye silaha kukishambulia ghafla kizuizi cha ukaguzi katika jimbo la magharibi la Anbar. Chanzo kutoka polisi ya Iraq kilisema kuwa washambuliaji waliokuwa na silaha mbalimbali walipambana na polisi katika mji wa Rawa.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment