Nchi ya Iran imewanyonga makachero wawili waliokuwa wakifanya kazi na shirika la ujasusi la Marekani (CIA) na lile la Israeli, Mossad.
Watu hao wawili ambao walihukumiwa adhabu ya kifo na Mahakama ya Mapinduzi ya Tehran, wamenyongwa leo Jumapili.
Jasusi wa Mossad, aliyetambuliwa kwa jina la Mohammad Heidari, alitiwa hatiani baada ya kukutwa na makosa ya kukusanya taarifa za Iran na kulipatia shirika la Ujasusi la Israeli katika mikutano mbalimbali nje ya Iran.
Heidari alikuwa akilipwa pesa na Mossad kwa kazi ya kuwafanyia ujasusi.
Jasusi mwingine, Kourosh Ahmadi, alitiwa hatiani kwa kushirikiana na CIA na kuwapatia taarifa za ujasusi zinazohusu Iran.
0 comments:
Post a Comment