MILIPUKO YAITIKISA MOGADISHU, 34 WAUAWA

A member of the Somali security forces walks past the site of a car bomb attack in central Mogadishu on March 18, 2013.
Mwanausalama wa Kisomali akitembea kwenye eneo lililoshambuliwa na bomu katikati ya mji wa Mogadishu Machi 18, 2013.



Watu wapatao 34 wamepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya milipuko kuutikisa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.



Baadhi ya waathirika walipoteza maisha yao baada ya bomu lililotegwa kwenye gari kulipuka mbele ya jengo la mahakama jirani na makao makuu ya utawala wa mji huo.


Kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya mlipuko huo, kundi la watu wenye silaha wakiwa wamevaa sare za jeshi la Somalia waliingia ndani ya mahakama hiyo, ambamo maafisa wa serikali walikuwa wamekusanyika, na kuanza kuwashambulia askari wa usalama ambao nao walijibu mapigo.


Mashuhuda hao wanasema kuwa walisikia milipuko isiyopungua miwili kutoka ndani ya jengo hilo. Vikosi vya serikali viliingia ndani ya jengo baada ya shambulio hilo na kumuokoa mwanasheria mkuu wa nchi hiyo.


Kundi la Al-Shabab limedai kuhusika na shambulio hilo.


Al-Shabab wameapa kuiangusha serikali ya Rais Hassan Sheikh Mohamud, aliyeingia madarakani mwezi Septemba, 2012 baada ya kuchaguliwa na bunge jipya la nchi hiyo.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment