Bibi wa miaka 90 amenusulika kufa baada ya matanki mawili ambayo kila moja linaweza kubeba rita 5000 kudondokea juu ya paa ya chumba anayoishi.
Matanki hayo yalidondoka toka ghorofa ya 13 kwenye jemgo la pembeni ambalo linaendelea kujengwa.
Ajari hiyo imetokea mtaa ulele(indhira ghandi) ambapo ghorofa lilianguka na kuua watu 36 mapema mwezi huu,
matanki hayo ambayo hayakuwekewa vizuizi vya kutosha yalidondoka toka ghorofa ya 13 mpaka juu ya paa ya nyumba ya jirani anapoishi bibi huyo,
Akielezea tukio hilo kwa masikitiko mtoto wa mama huyo alisema "tukio hili si mara ya kwanza kutokea , wakati hili jengo lipo ghorofa ya ya kumi lilidondoka tofari na vipande vya nondo na kupenya katika paa kama yalivyo penya matenki"
hii ni mara ya pili kudondokea chumba hiki, tunaiomba serikali ije mapema kulikagua jengo hili maana linatupa wasiwasi aliongeza kijana huyo mwenye asili ya asia.
Mpaka sasa mzizima 24 haifahamu hatua gani zimechukuliwa na serikali.
0 comments:
Post a Comment