AFGHANISTAN: MAFURIKO YASABABISHA MAAFA




Idadi ya vifo kutokana na mafuriko makubwa ya hivi punde kufuatia mvua kubwa kaskazini mwa Afghanistan imegharimu maisha ya watu 20.



Afisa katika ofisi ya gavana wa jimbo la Balkh, bwana Zabihullah Akhtari, anasema kuwa karibu kaya 2,000 zimeathiriwa katika mji mkuu wa jimbo hilo wa Mazar-i-Sharif - unaopatikana kilometa 300 (maili 186 ) kaskazini magharibi mwa Kabul - na miji mingine mitatu ya jirani.



Aliongeza kuwa watu 8 walipoteza maisha katika wilaya ya Sholgara, saba mjini Kishindih, wanne mjini Charkint na mmoja mjini Mazar-i-Sharif. 


"Mifugo na nyumba zetu vyote vimeharibiwa," Ghulam Sakhi, mkazi wa kijiji kimoja katika wilaya ya Sholgara alisema. "Mafuriko yalikuwa makubwa sana kiasi kwamba tulishindwa kufanya chochote." 

Wakati huo huo, mkuu wa wilaya ya Sholgara, Maulvi Sirajuddin Abid, amesema kuwa kiasi cha nyumba 1,300 zimeathiriwa kutokana na gharika hiyo. Alieleza pia kuwa karibu ekari  2,500 za ardhi ya kilimo zimeharibiwa vibaya sana.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa mafuriko yamefunga barabara kuu za jimbo la Balkh.


Jana Jumatano asubuhi, mvua kubwa ilisababisha mafuriko kama hayo katika jimbo jirani la Sari Pul na kuharibu zaidi ya nyumba 100.



Eneo la kaskazini mwa Afghanistan linakabiliwa na mvua nzito isiyokuwa ya kawaida na kusababisha mafuriko.


Nyumba nyingi katika vijiji vya Afghanistan zimejengwa kwa udongo au mawe, na hivyo kuwa rahisi sana kusombwa na mafuriko.


Masika iliyopita, idadi kubwa ya watu walipoteza maisha kwa mafuriko kaskazini mwa Afghanistan.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment