Ndege za kivita za Israeli aina ya F-16 |
Jeshi la Israeli limesema kuwa limetungua ndege isyokuwa na rubani (drone) inayomilikiwa na Hezbollah karibu na bandari ya kaskazini ya Haifa.
Ndege iliyokuwa imembeba Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, ambaye alikuwa akifanya ziara katika eneo la kaskazini la nchi hiyo, ililazimishwa kutua kufuatia hatua ya 'drone' hiyo kuingia katika anga la Israeli.
Katika taarifa yake, Netanyahu alisema kuwa tukio hilo ni “zito mno.”
Inaelezwa kuwa meli za Israeli zinatafuta mahali ndege hiyo ilipodondokea.
Aidha, mwezi Oktoba, mwaka jana, ndege kama hiyo iliyotumwa na Hezbollah ilipenya ndani kabisa ya Israel kabla ya kuangushwa na makombora ya Israeli.
0 comments:
Post a Comment