Wakuu wa Afrika wasaini mapatano ya amani ya Kongo

Wakuu wa Afrika wasaini mapatano ya amani Kongo



Wakuu wa nchi za Kiafrika wamesaini makubaliano ya kurejesha amani na utulivu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Zoezi hilo limefanywa na viongozi hao wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia. Ban Ki moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye amehudhuria sherehe hizo amekaribisha makubaliano hayo na kueleza kuwa, mapatano hayo yanamaanisha kuanza kiapo cha pamoja cha ulazima wa kuheshimu nchi za eneo la maziwa makuu, suala la kurejesha amani na utulivu katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa na maliasili za madini.  

Waasi wa Machi 23 wa mkoa wa Kivu Kaskazini tarehe 27 Novemba mwaka jana waliondoka huko Goma makao makuu ya mkoa huo kutokana na mashinikizo ya viongozi wa nchi za eneo hilo na jamii ya kimataifa, hata hivyo waasi hao wanaendelea kudhibiti maeneo mengi huko Kongo.  Nchi 14 wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC zimeshiriki kwenye utiaji saini makubaliano hayo zikiwa kama wapatanishi.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment