VITA YAZOROTESHA ELIMU YA WATOTO NCHINI MALI

Malian refugee children sit on December 7, 2012 under a tent that serves as a classroom in the Goudebou refugee camp, some 20 kilometers from the northwestern Bukinabe city of Dori.
Watoto wa Mali waliokimbia vita wakiwa wamekaa chini ya hema linalotumika kama darasa katika kambi ya wakimbizi ya Goudebou, kiasi cha kilometa 20 kutoka kaskazini-magharibi mwa mji wa Bukinabe huko Dori.



Shiriki la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto (UNICEF) linasema kuwa vita inayoendelea nchini Mali imezorotesha hali ya elimu nchini humo.


Mnamo Januari 11, Ufaransa ilianzisha vita nchini humo kwa hoja ya kuwazuia waasi wasisonge mbele baada ya kulidhibiti eneo la kaskazini mwa nchi hiyo. Marekani, Canada, Uingereza, Ubelgiji, Ujerumani na Denmark zimeunga mkono hatua hiyo.


"Walimu wengi wameshindwa kurudi kaskazini na tayari shule za kusini zimeshaelemewa na mzigo na haziwezi kustahmili wimbi la wanafunzi kutoka kaskazini waliokimbia mapigano," UNICEF ilisema katika taarifa yake iliyoitoa jana Jumapili.



Wakati huo huo, Francoise Ackermans, mwakilishi wa UNICEF nchini Mali anasema kuwa "Mwalimu anapoogopa kufundisha na mwanafunzi anapoogopa kwenda shule, mfumo wote wa elimu huwa hatarini."


Hali hii inatokea huku Waziri wa Elimu wa Mali, Bocar Moussa Diarra akisema kuwa ni shule tatu pekee kaskazini mwa Mali ndizo zinazofanya kazi.


Waziri huyo amebainisha kuwa katika mji wa kaskazini wa Kidal, shule zote zimefungwa ilhali katika mji wa Timbuktu ni asilimia tano tu ya shule ndizo zimefunguliwa upya.

“Katika mji wa Gao, asilimia 28 tu ya walimu ndio walioanza kazi," alisema na kuongeza kuwa "mamia ya shule yanahitaji kujengwa au kukarabatiwa, na kuwekewa vifaa vya shule."


Vita hiyo inayoongozwa na Ufaransa imesababisha mgogoro mkubwa sana wa kibinaadamu katika maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo, maelfu ya watu hawana makazi, na wanaishi katika hali mbaya sana.


Watu wa kasikazini mwa Mali wanasema kuwa vita hiyo inakwaza ufikaji wa misaada ya kibinaadamu katika maeneo yaliyoathiriwa na vita.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment