![]() |
| Katika picha hii, wafanyakazi wa huduma ya dharura wakiwa upande wa mbele wa ubalozi wa Marekani baada ya shambulio la mlipuko katika ubalozi huo mjini Ankara, Uturuki, leo Februari 1, 2013. |
Vyombo vya habari nchini Uturuki vimeripoti kuwa pametokea mlipuko nje ya ubalozi wa Marekani mjini Ankara, Uturuki na kuua walinzi wasiopungua wawili.
Mashuhuda wamenukuliwa wakisema kuwa mlipuko huo ulitokana na mtu aliyejilipua.
Magari ya wagonjwa na yale ya kuzima moto yalielekea haraka eneo la tukio.
Katika eneo hilo kuna balozi nyingine kadhaa za nchi mbalimbali.
Mwaka 2008, watu watatu waliokuwa na silaha na polisi watatu waliuawa katika shambulio lililotokea katika ofisi za ubalozi mdogo mjini Istanbul.

0 comments:
Post a Comment