Wahamiji haramu wanaoingi nchini hatimaye wametoa sababu zao za msingi zinazowafanya kuingia nchini ambazo ni pamoja na malipo bora toka kwa waajili mashambani na hali ya usalama nchini.
Kijiji cha Igate Kata ya Nzela wilayani Geita ambacho wananchi wake wanajihusisha na kilimo cha Nanasi ndio wanaoongoza kwa kuajiri wahamiaji haramu na kuwatumia kama vibarua.
Ni mmoja wa wahamiaji haramu kumi walikamatwa katika kijiji cha Igate Mkoani Geita katika Operesheni maalumu inayoendeshwa na idara ya uhamiaji kupambana na wahamiaji haramu akielezea sababu zake za msingi kuingia nchini kinyemela.
Katika kijiji cha Igate Mkoani Geita Idara ya Uhamiaji imeanzisha Elimu elekezi kuwaeleza wananchi madhara ya wahamiaji haramu.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Manguchie anasema Serikali ya Tanzania haizuii wahamiaji bali wanapaswa wafuate taratibu zilizowekwa kimataifa
Maafisa Uhamiaji wa Idara wa Uhamiaji Geita Vitalis Komanya na Maria Lucas wamebainisha wazi kuwa wananchi wanatakiwa kubuni mikakati endelevu ya kuendesha kilimo bila ya kutegemea wahamiaji haramu na kuwafichua mara wanapowabaini.
Kaimu Afisa uhamiaji Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Charles Washima amesema Idara hiyo sasa itabadili mfumo kwa kuwakata na kuwafikisha mahakamani wahamiaji haramu na wale wanaowahifadhi
Kwa mujibu wa sheria ya uhamiaji ya mwaka 1995,mtu anayekutwa amemwajiri mhamiaji haramu atakuwa ametenda kosa la jinai.
CHANZO: STAR TV
0 comments:
Post a Comment