MGOMBEA URAIS APIGWA RISASI


Wauguzi wakimbemba mgombea wa kiti cha Urais wa Armenia, Paruir Airikian, kwenye hospitali moja mjini Yerevan, Armenia, leo Februari 1, 2013.



Polisi nchini Armenian wamesema kuwa mtu mmoja aliyekuwa na silaha amempiga risasi na kumjeruhi mmoja wa wagombea nane wa kiti cha Urais nchini humo.

Mamlaka zinasema kuwa Paruir Airikian alipigwa risasi na mshambuliaji ambaye hakutambuliwa jana Alhamisi katika mji mkuu wan chi hiyo, Yerevan.

Maafisa wanasema kuwa Airikian, mwenye umri wa miaka 63, yuko katika hali ya kuridhisha.

Kwa mujibu wa sheria za Armenia, kampeni za urais inaweza kuakhirishwa kwa muda wa wiki mbili iwapo Airikian, mpinzani wa zamani, hataweza kuendelea na kampeni.

Rais wa sasa, Serzh Sarkisian anatarajiwa kushinda uchaguzi wa urais utakaofanyika Februari 18.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment