![]() |
| WATU WAKIKIMBIA KUELEKEA KWENYE TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA ENEO LA KIKABILA LA ORAKZAI, KWENYE MPAKA WA PAKISTAN NA AFGHANISTAN. |
Kwa uchache watu 10 wameuawa na zaidi ya 23 kujeruhiwa katika shambulizi la bomu lililolenga soko moja katika eneo la kaskazini magharibi mwa Pakistan la Orakzai.
Tukio hiyo limetokea leo Ijumaa baada ya bomu lililotegwa jirani na ofisi za serikali na za usalama kulipuka katika soko hilo la mji wa Kalaya katika jimbo la Orakzai.
Mlipuko huo umeripotiwa kuharibu duka moja katika soko hilo, huku maafisa wa eneo hilo wakisema kuwa baadhi ya majeruhi wako katika hali mbaya.
Orakzai ni moja ya maeneo yanayoshuhudia makabiliano ya kimapambano kwenye mpaka wa Afghanistan ambapo wanajeshi wamekuwa wakipambana na wanamgambo wenye uhusiano na Taliban.
Jeshi lilianzisha operesheni nyingi dhidi ya wapiganaji hao tangu mwaka 2009, lakini wanamgambo hao wameendelea kufanya mashambulizi kadhaa wa kadhaa yasiyotarajiwa.

0 comments:
Post a Comment