AMUUA KINYAMA DADA YAKE MJAMZITO KWA KISINGIZIO CHA KULINDA HESHIMA


The body of 18-year-old Baghdad Khaled al-Issa, who was killed by her brother, lies on the ground in Wazzani, south Lebanon, Friday, Feb. 8, 2013. (The Daily Star/Stringer)
Mmwili wa Baghdad Khaled al-Issa, aliyeuawa na kaka yake, ukiwa umelala chini katika mkioa wa Wazzani, kusini mwa Lebanon, leo Ijumaa Feb. 8, 2013.



Duru za Usalama nchini Lebanon zimeeleza leo kuwa binti mmoja mjamzito ameuawa na ndugu yake kusini mwa nchi hiyo katika kile kinachoelezwa na polisi kuwa ni kadhia ya “mauaji ya heshima”.

Mwili wa Baghdad Khaled al-Issa mwenye umri wa miaka 18 ulipatikana Alhamisi Usiku katika mkoa wa mpakani wa kaskazini wa Wazzani.

Maafisa wanasema kuwa mwili huo ulikutwa katika dimbwi la damu huku ukiwa na majeraha makali kichwani na mbavuni.

Uchunguzi wa polisi umebaini kuwa binti huyo aliuliwa na kaka yake, Jihad, katika kile kinachoitwa kama mauaji kwa ajili ya "heshima ya familia”family honor".

Chanzo kimoja cha usalama kimesema kuwa binti huyo alikuwa na ujauzito wa miezi saba.
Mnamo Agosti 2011, wabunge wan chi hiyo walipitisha sheria ya kuongeza adhabu dhidi ya kinachodaiwa kuwa ni “uhalifu wa heshima.”

Sheria hiyo inataka kufutilia mbali kanuni ya adhabu  inayotoa tahfifu ya adhabu kwa yeyote anayemuua mke, mume au mwanafamilia wa karibu anayekutwa katika tukio la uzinifu kwa hoja kwamba kisingizio cha kusukumwa na hasira.



Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment