APOTEZA MENO YOTE BAADA YA KUNYWA LITA 8 ZA COLA KWA SIKU



Replacement teeth: Mr Kennewell has had a full set of dentures fitted to replace his teeth which have rotted because of the amount of cola he consumed each day
MENO MBADALA: BWANA KENNWELL ALIWEKEWA JOZI KAMILI YA MENO BANDIA BAADA YA MENO YAKE YA ASILI KUOZA KUTOKANA NA KUTUMIA KIWANGO KIKUBWA CHA COLA KWA SIKU.

Kijana mmoja aliyetopea katika unywaji amepoteza meno yake yote baada ya kuwa na tabia ya kunywa lita nane za cola kwa siku.

Kijana huyo, William Kennewell raia wa Australia, mwenye umri wa miaka 25, na ambaye ni mfanyakazi wa hoteli alipuuzia maonyo na tahadhari mbalimbali alizokuwa akipatiwa na madaktari wa meno kwamba tabia yake hiyo ingeyaharibu meno yake. Sasa amepoteza meno yake yote katika umri wa ujana wa miaka 25.
Tabia ya bwana Kennewell ya kupenda vinywaji vyenye sukari imemfikisha mbali zaidi kiasi cha kumuachia sumu katika damu yake.

Anasema: “Nilikunywa lita sita mpaka nane za vinywaji laini, hasa cola, kila siku.
Nimeeambiwa kuwa mtu wa kawaida anakuwa na takriban meno 23,  lakini nimebaki na meno 13 ambayo yanatakiwa kung’olewa,” alimwambia mwandishi wa habari katika mji wa Adelaide.

Ukweli ni kwamba wengi katika watu wazima huwa na meno 28 au 32, kutegemea na jinsi wanavyoyajali meno yao, jambo linaloonesha kuwa jamaa huyo atakuwa na wakati mgumu sana.

Bwana Kennewell, anayesishi Salisbury, maili 15 kaskazini mwa mji wa Adelaide, aliongeza kusema: “Ilitokea kwa sababu sikuwa mpenzi mkubwa wa maji na kazi yangu katika tasnia ya hoteli ilinifanya niwe na fursa ya kutumia sana Coke.

Kwa kuwa meno yangu yalikuwa yakioza sana, ilisababisha sumu katika damu iliyonifanya nianze kuumwa- lakini afya yangu iliimarika baada ya kupatiwa meno bandia.”

Wataalamu wa afya nchini Australia wanatumia tukio la Kennewell kama mfano halisi kuwaeleza vijana kwa nini wanatakiwa kuepuka unywaji wa kupindukia.

Dr Jason Armfield, mtafiti mwandamizi katika kituo cha Australian Research Centre for Population Oral Health amependekeza yawekwe maonyo ya kiafya kwenye nembo za vinywaji laini vinavyoongeza hatari ya meno kuoza.

Ameshafanya utafiti kati ya watoto 16,800 wa Australia uliobaini kuwa asilimia ya 56 watoto wenye umri wa kati ya miaka 5 na 16 walitumia angalau kinywaji kimoja kitamu – kinywaji laini au juisi – kila siku.

Bwana Kennewell alikubali kwamba kuweka maonyo ya kiafnya kwenye vinywaji laini ni wazo zuri- lakini akahoji yatakuwa na athari kwa kiwango gani.

CHANZO: DAILY MAIL

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment