HALI YA KIBINAADAMU NCHINI MALI YAZIDI KUWA MBAYA


French soldiers are seen at an airbase near Bamako, Mali. (File photo)


Katikati ya ripoti za unyanyasaji, dhulma na ukosefu wa chakula kaskazini mwa Mali, watu wengi katika nchi hiyo wanaamini kuwa vita hiyo inayoongozwa na majeshi ya Ufaransa imezidisha hali ya mambo kuwa mabaya.

Wananchi wa Mali kaskazini wanalalamika kuwa wamepuuzwa na mamlaka wakati wakiwa katika hali  mbaya ya ukosefu wa chakula, maji na huduma za afya.

“Nina wasiwasi mno...," alisema mkazi mmoja, akielezea matukio ambayo ameyashuhudia kwa macho yake katika wiki kadhaa baada ya vita.

Ufaransa ilianzisha vita dhidi ya Mali mnamo Januari 11 kwa hoja ya kupambana na waasi wa nchi hiyo waliokuwa wakizidi kusonga mbele katika kampeni yao ya kijeshi. Vita hiyo imewaacha maelfu ya wanachi wa Mali bila makazi.

Ripoti zinasema kuwa wazee katika vijiji vya ndani wana hali ngumu sana kutokana na tatizo la ukosefu wa chakula.

Mnamo Februari 1, Shirika la Amnesty International lililaani “ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu" ikiwemo mauaji ya watoto katika vita hiyo.

Shirika hilo la haki za binaadamu lilisema kuwa kuna “ushahidi kwamba kwa uchache raia watano, wakiwemo watoto watatu, waliuawa katika shambulizi la ndege" lililofanywa na majeshi ya Ufaransa dhidi ya waasi.

Wachambuzi wanaamini kuwa nyumba ya kampeni hii ya kijeshi kuna suala la maliasili za nchi hiyo kama vile mafuta, dhahabu na madini ya urani.

Hali ya kibinaadamu nchini Mali baada ya kuanza kwa vita hiyo ya Ufaransa imezidi kuwa mbaya na kuwalazimu maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao.

Kiasi cha watu 380,000 wameachwa bila makazi wakati huu ambapo vita hiyo imeingia wiki ya tano.

Karibu wakimbizi 700000 wa Mali wanaishi katika kambi moja ya wakimbizi nchini Niger tangu Januari 11.

sanjari na Niger, nchi za Mauritania na Burkina Faso nazo zimewapa hifadhi wakimbizi wa Mali.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment