![]() |
Wahispania wakiandamana nje ya bunge kupinga sheri kali za rehani, Februari 12, 2013. |
Wanandoa wawili nchini Hispania wamejiua baada ya kupokea amri inayowataka kuihama nyumba yao katika kisiwa cha Mediterranean cha Mallorca kutokana na kushindwa kulipa deni.
Saa kadhaa baada ya tukio hilo, bunge la Hispania lilipiga kura ya kupitia upya sheria ngumu na kali za mikopo ya nyumba na rehani katika nchi hiyo. Sheria hiyo inayosubiri kupitishwa na bunge, ingeruhusu wamiliki waliofilisika kufuta madeni yao kwa kunyang'anywa mali zao. Lakini, mjadala mkali uliendelea kwa miezi kadhaa au miaka mingi bila hata kufanyiwa marekebisho.
Chini ya sheria ya sasa, wamiliki wanaofukuzwa bado wanaweza kulipa kiwango kikubwa cha deni hata kama thamani ya nyumba yao itakuwa imeshuka kwa kipindi cha miaka minne kabla.
Mnamo Novemba 2012, serikali ya Hispania ilisitisha suala la wamiliki kuondolewa katika makazi yao kwa miaka miwili kutokana na maandamano ya wananchi na kukithiri kwa matukio ya watu kujiua. hata hivyo, sheria hiyo ina masharti ambayo yanazihusu familia chache za Wahispania.
Tangu Novemba 2012, juma la ya watu 5 wamejiua kutokana na kushindwa kulipa rehani na suala la kuondoshwa kwenye makazi yao.
Mkasa wa kudorora kwa uchumi wa dunia, uchumi wa Hispania ulianguka katika nusu ya pili ya mwaka 2008 na mamilioni ya watu wakapoteza kazi zao.
Tokea mdodoro huo ulipoanza, zaidi ya Wahispania 350,000 wamepokea amri za kuondoka kwenye nyumba zao.
Hispania inapaswa kupunguza nakisi ya bajeti yake mpaka asilimia 4.5 mwaka 2013 na asilimia 2.8 mwaka 2014. Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya uchumi wanasema bado kuna ugumu wa kufikia malengo hayo kutokana na matarajio hafifu ya kuimarika kwa uchumi wa nchi hiyo.
0 comments:
Post a Comment