BUNGE LA UFARANSA LAIDHINISHA NDOA ZA JINSIA MOJA


Bunge la Ufaransa laridhia ndoa ya watu wa jinsia moja


Bunge la wawakilishi nchini Ufaransa limeidhinisha muswada unaoruhusu ndoa ya watu wa jinsia moja licha ya upinzani mkali kutoka kwa makundi ya kidini, mashirika ya kijamii na vyama vya mrengo wa kulia. Muswada huo umepitishwa kwa kura 320 dhidi ya 299 za kuupinga. 

Mashirika ya kidini na yale ya kijamii yamesema taasisi ya familia inaelekea kusambaratika nchini Ufaransa na yametoa wito kwa bunge la Senate kuutupilia mbali muswaada huo mwezi Aprili mwaka huu. 

Kifungu cha katiba ya Ufaransa kinachotambua ndoa kuwa uhusiano wa kimapenzi kati ya mwanaume na mwanamke kimebadilishwa na sasa kinatambua ndoa kuwa uhusiano wa watu wawili. Rais Francois Hollande ameahidi kuunga mkono muswada huo utakapopelekwa katika bunge la Senate ili kupigiwa kura ya mwisho.

 Iwapo utapitishwa na kuwa Sheria basi Ufaransa itakuwa imejiunga na nchi zingine za Ulaya kama vile Uholanzi, Ubelgiji, Denmark, Ureno, Norway, Uhispania, na Sweden ambazo tayari zimeidhinisha uozo huo unaopingwa na dini zote za mbinguni.

CHANZO: IRIB
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment