MKAZI wa Kijiji cha Idunda, Kata ya Kifanya wilayani Njombe, Leonald Mapile (25), amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumbaka na kumjeruhi sehemu zake za siri mtoto wake mwenye umri wa miaka sita.
Akisoma kesi hiyo iliyovuta hisia za wakazi wengi wa mji wa Njombe, mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe, Isack Mlowe, Mwendesha Mashitaka, Henry Chaula, alidai mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 22, 2012, saa saba mchana nyumbani kwao.
Alidai mshitakiwa alimwingilia kimwili mtoto huyo na kumsababishia majeraha katika sehemu zake sa siri.
Hata hivyo, mshitakiwa huyo alikana mashitaka yanayomkabili na amerudishwa mahabusu hadi kesi yake itakapotajwa tena Februari 6, mwaka huu.
Katika tukio jingine, Christina Mtulo (19), amekutwa amekufa baada ya kubakwa kabla ya kuuawa na kundi la watu wasiofahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Fulgence Ngonyani, alisema tukio hilo limetokea juzi maeneo ya Mgendela, Njombe Mjini na baada ya mwanamke huyo kuuawa mwili wake ulitupwa katika kibanda cha mgahawa.
Alisema hakuna aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo na wanaendelea kufanya uchunguzi.
Wakati huohuo, Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamsaka mwanaume asiyejulikana kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, alisema tukio hilo limetokea Ipogoro B, Manispaa ya Iringa ambapo mwanaume huyo alimvamia mtoto huyo na kumbaka kisha akatoroka.
“Hatujamjua ni nani lakini atapatikana tu kwa sababu hii ni hatari na amefanya hivi kutokana na tamaa zake za mwili, si vinginevyo,” alisema Kamuhanda.
CHANZO: MTANZANIA
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment