![]() |
| Rais wa Ufaransa Francois Hollande |
Rais wa Ufaransa Francois Hollande amewasili nchini Mali takriban wiki nne baada ya Ufaransa kuanzisha uperesheni ya kijeshi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
"Ninakwenda Mali kuwaunga mkono, kuwashajiisha na kuwaonesha kuwa tunaona fakhari kwa kazi yao," alisema kabla ya kuanza ziara yake.
"Vilevile ninakwenda kuhakikisha majeshi ya Afrika yanakuja na kuungana nasi haraka iwezekanavyo na kuwaambia kuwa tunawahitaji katika kikosi hiki cha kimataifa."
Wakati huohuo, siku ya Ijumaa, Shirika la Amnesty International lilitoa wito kwa jeshi la Ufaransa kuanzisha uchunguzi wa vifo vya raia watano wa Mali, akiwemo mwanamke mmoja na watoto watatu waliokufa katika shambulio la helikopta lililofanywa na majeshi ya Ufaransa dhidi ya mji wa Konna siku ya kwanza kabisa ya vita hivyo.
Pia, Shirika hilo la haki za binaadamu lenye makao yake mjini London lilitoa shutumakwa jeshi la Mali kwa kuwaua raia 20 kaskazini mwa nchi hiyo.
Mnamo Januari 11, Ufaransa ilianzisha vita dhidi ya Mali kwa kisingizio cha kuwazuia wapiganaji wanaoipinga Serikali wasisonge mbele katika mapigano yao.
Siku nne baadaye, Ufaransa ilitangaza kuwa ingeongeza wanajeshi mara tatu kutoka wanajeshi 800 mpaka 2500. Wanajeshi wa Ufaransa walianzisha mashambulizi ya ardhini Januari 16.

0 comments:
Post a Comment