Ripoti: Sarkozy alipokea ‘€50 milioni’ kutoka kwa Qaddafi


Sarkozy and Qaddafi pictured in Paris in 2007. (Reuters)
Sarkozy na Qaddafi katika picha  mjini Paris mwaka 2007.


Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy alichukua zaidi ya €50 milioni kutoka kwa kiongozi wa za zamani wa Libya, marehemu Kanali Muammar Qaddafi, repoti moja iliyotolewa Siku ya Alkhamisi imefichua.

Mfanyabiashara mwenye asili ya Lebanon, Ziad Takieddine alimwambia jaji mmoja mpelelezi kuwa ana "uthibitisho wa maandishi" ya uhamishwaji wa fedha kutoka kwa Gaddafi na mwanae mmoja wa kiume kwenda kwa Sarkozy ambao ni zaidi ya €50 milioni zilizotolewa mfumo usio halali, gazeti la Uingereza la the Independent limeripoti.

Fedha hizo zilitumiwa na Sarkozy kusaidia kampeni yake ya kwanza ya urais mwaka 2006-7, ambayo  ilifadhiliwa "sana" na Tripoli na kuendelea mpaka kabla ya kuanguka kwa utawala wa Libya, ambayo ilishambuliwa kwa sehemu kubwa na ndege za Ufaransa na Uingereza mwaka 2011.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, vyanzo vilivyo karibu na Takieddine, vimezielezea tuhuma hizo kuwa ni za "kifisadi" na "maslahi binafsi."

Tuhuma sawa na hizo ziliibuka mwezi Aprili mwaka 2012. Msemaji wa wakati huo wa kampeni ya Sarkozy, Nathalie Kosciusko-Morizet ameikanusha ripoti hiyo na kuiita kuwa ni ya "kipuuzi" na "upotoshaji mkubwa" uliopikwa na kambi ya Hollande’s camp.

Katika baruapepe moja kwenda shirika la habari za AFP, alisema kuwa fedha za kampeni ya  Sarkozy ya mwaka  2007 zimeshachungwa na Baraza la Katiba baada ya uchaguzi na kubainika kuwa hazikuwa na kasoro.

Nyaraka ya mwaka 2006 iliyo katika lugha ya Kiarabu, ambayo tovuti ya Mediapart ilisema kuwa ilisainiwa na mkuu wa upelelezi wa nje wa Gaddafi, Mussa Kussa, inaelezea “makubaliano ya msingi ya kusaidia kampeni kwa ajili ya mgombea  urais, Nicolas Sarkozy, yenye thamani ya yuro milioni 50."

Uchunguzi wa tovuti hiyo ya mrengo wa kushoto ulitoa madai kama hayo mnamo Machi 12, kwa ushahidi uliotolewa na dkatari wa zamani wa mfanyabiashara wa silaha raia wa Ufaransa aliyedaiwa kuratibu ufadhili huo wa kampeni. 

Takieddine, ambaye yuko katikati ya madai haya mapya, "amekuwa mratibu wa mahusiano halani na ya haramu baina ya Ufaransa na Mashariki ya Kati kwa muda wa miaka 20," linasema gazeti la the Independent.

Lakini yeye mwenyewe yuko chini ya uchunguzi rasmi "kwa kuratabu na kupokea fedha chafu katika biashara ya silaha kwa kipindi cha zaidi ya miongo miwili," lilisema gazeti hilo.

Katika maelezo aliyoyatoa katika gazeti la Le Parisien, alisema kuwa tuhuma hizo dhidi ya Sarkozy ni sehemu ya makubaliano na mfumo wa mahakama wa Ufaransa. Kwa mujibu wa maelezo yake, makubaliano hayo yatajumuisha kuwachunguza wanasiasa wa Ufaransa waliofadhiliwa na Libya.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment