![]() |
| Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano ya Umma CUF – Taifa- Abdul Kambaya |
PROF.MUHONGO AMEPOTOSHA UKWELI WA MADAI YA WANANACHI WA MTWARA
03/01/2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
CUF-Chama cha Wananchi Kimesitushwa na tamko la Serikali, lililotolewa na Prof Muhongo kuhusu Maandamano yaliofanywa na Wakazi wa Mtwara, ili kuishinikiza Serikali kuweza kutumia Gesi ilopatikana Mtwara kujenga Viwanda vitakavyoongeza Ajira kwa watu wa Mtwara. Serikali imekuja juu na kutoa kauli kwamba Gesi iliopatikana Mtwara ni % 14 na Lindi ni % 7 na %78 inapatikana kwenye Bahari ya kina kirefu na Pwani ni % 1 inapatikana kwenye Bahari ya kina kirefu na kwa hivyo si busara kwa Wakazi wa Mtwara kudai kujengwa kwa Viwanda kwa kutumia Gesi hiyo.
Hata hivyo Prof Muhongo hakusema hiyo % 78 inayopatikana kwenye kina kierefu cha Bahari kipo kwenye Mkoa gani ?. CUF – Chama cha Wananchi kinatilia shaka kauli hiyo na kauli nyingine iliosema kwamba, mbona mapato ya Dhahabu na Tanzanite na umeme unaozalishwa na kwenye Mikoa ya Mororogo na Maji ya Ruvu yanatumika maeneo mengine. Hoja hizi ni dhaifu kwakua, hoja ya watu wa Mtwara, si kuitumia Gesi au mapato yatokanayo na Gesi, Hoja ya watu wa Mtwara ni kwamba, wanaihitaji Serikali kujenga Viwanda vitavyotumia gesi kwenye Mkoa huo ili kuongeza Ajira kwa watu wa Mkoa huo.
CUF- Chama cha Wananchi, kinahoji, kwa nini Kiwanda cha Makaa ya Mawe hakijajengwa Dar es Salaam, kwa nini Usafishaji wa Dhahabu haufanyiki Dar es Salaam na badala yake unafanyika kwenye Maeneo yanapopatikana Dhahabu kama vile Mbeya kwenye Makaa ya Mawe, Mwanza, Arusha,Shinyanga,Geita, Mara na Maeneo mengine. Watu wa Mtwara wanaendeleza utaratibu ule ule uliosasisiwa na Serikali wa kuacha dhahabu iliogunduliwa kwenye maeneo ya Mwanza,Arusha,Mara,Geita,Shiny
CUF- Chama cha Wananchi kinatoa wito kwa Serikali juu ya kutimiza ahadi ya Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ya kujengwa kwa Viwanda Mikoa ya Mtwara na Lindi ili kuongeza ajira kwa wakazi wa Mikoa hiyo. Prof Muhongo anapaswa kukumbuka ahadi iliotolewa na Rais na kusiwe na majibu mepesi kwenye hoja na ahadi ya msingi ilotolewa na Rais.
Imetolewa na Abdul Kambaya Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano ya Umma CUF – Taifa
About mahamoud
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:
Post a Comment