maaskofu mashoga waruhusiwa- lakini hawatakiwi kuoa




Usiku wa jana Kanisa la Kianglikana Uingereza limeibua upya mjadala kuhusu suala zito katika kanisa hilo kwa kusema wazi kuwa mashoga wanaweza kuwa maaskofu, iwapo watakuwa waseja na kama hawataoa.

Tangazo hilo ambalo halikutarajiwa liliwashangaza na kuwashtua sana wale wanaunga mkono na wale wanaopinga mashoga kufanya kazi ya uaskofu, na uamuzi huo unatishia kumletea shida Askofu Mkuu ajaye, Justin Welby,  na kuibua mgogoro mpya na mzito ndani ya kanisa hilo.

Kiongozi mmoja mwenye mrengo wa kihafidhina alionya kuwa hatua hiyo italiibua suala la maaskofu wanawake na "hatimaye kuligawa kabisa Kanisa la Anglikana".

Japokuwa waliberali wamezipokea habari hizo, nao pia wameelezea wasiwasi wao kwamba maaskofu mashoga bado watatakiwa kujibu maswali tata kuhusu suala la useja-kitu ambacho wenzao wasiooa hawatarajiwi kukifanya. Suala la kuwasimika watawa mashoga kuwa maaskofu limesababisha mgawanyiko mkubwa ndani ya Kanisa tangu Jeffrey John alipolazimishwa kuacha kuwania uaskofu wa mji wa Reading mwaka 2033, kufuatia kilele za watawa wenye mrengo wa kihafidhina.

Uamuzi wa jana unaweza kumtengenezea njia Dr John, ambaye kwa sasa ni mwalimu katika chuo cha St Albans na ambaye ni katika watawa wachache wanaofanya ushoga waziwazi lakini hawana wake, kushika wadhifa mkubwa ndani ya Kanisa.

Mwaka 2005, Kanisa liliamua kuwa mtu mwenye uhusiano wa jinsia moja angeweza kuwa mtawa, lakini halikusema chochote kuhusu mtu huyo kama anaweza kuwa askofu.

Mwaka 2011, viongozi wakuu wa Kanisa walisitisha mpango wowote wa kuwapandisha hadhi watawa kuwa maaskofu baada ya wahafidhina kutishia kuligawa kanisa hilo vipande viwili.

Na sasa baraza la Maaskofu, chombo rasmi chenye majukumu ya mafundisho ya kanisa, limeondosha marufuku hiyo kwa kutangaza kuwa ushoga hauwezi kuwa kizuizi cha watu kuwa maaskofu.

Hatua hiyo imekuja baada ya wiki kadhaa za shutuma dhidi ya kanisa kwenye suala la jinsia baada ya mwezi wa Novemba kushindwa kupitisha sheria inayowaruhusu wanawake kuwa maaskofu na tangazo la Serikali mwezi uliofuatia kuwa Kanisa halitahusika katika sheria ya ndoa za jinsia moja.

Uamuzi huo wa Baraza la Maaskofu, ambao ulichukulia tangu mwezi wa Disemba lakini ukaja kujulikana hapo jana, unahitimisha marufuku iliyowekwa kwa mtu anayefanya ushoga wazi wazi kuwa askofu ilimradi asiowe.

Dr Welby anaupeleka msimamo wa wahafidhina kwenye ushoga lakini Askofu Mkuu anaweza akakabiliana na mgogoro wa moja kwa moja kutoka kwenye Baraza la Maaskofu mara atakapoanza kazi yake. Uteuzi wake ulipotangazwa alisema kuwa angeutazama upya msimamo wake kuhusu ushoga "kwa ibada na umakini". 

Usiku wa jana, Askofu wa Norwich, Rt Rev Graham James, alisema: "Baraza limethibitisha kuwa watawa walio katika uhusiano wa jinsia moja na kuishi kwa mujibu wa mafundisho ya Kanisa juu ya uhusiano wa kijinsia, wanaweza kuwa maaskofu. Baraza liliamini kuwa haitakuwa haki kumuengua mtu anayetaka kuishi kikamilifu kulingana na mafundisho ya Kanisa juu ya maadili ya uhusiano wa kijinsia au maeneo mengine ya maisha binafsi ya mtu."

Askofu huyo aliongeza kuwa kwa sababu ya utata unaouzunguka uteuzi huo, mtawa yeyote shoga anayetaka kuwa askofu anatarajiwa kujibu maswali kuhusu useja wake.

Hatua hiyo itasababisha mawimbi nje ya mipaka ya Uingereza. Kanisa la Uingereza ndio makao makuu ya kanisa la Anglikana lenye wafuasi milioni 80 waliotapakaa duniani kote ambao wamekuwa na maoni tofauti kuhusu masuala ya msingi kama vile wanawake na ushoga. Mchungaji Rod Thomas, ambaye ni mwenyekiti wa Kundi la Maaskofu wenye mrengo wa kihafidhina, alionya kuwa uteuzi wowote wa kumfanya shoga kuwa askofu utaleta "mgawanyiko mkubwa". "Itaibua migawanyiko kuhusu suala la  maaskofu wanawake," aliliambia gazeti la The Independent. "Kanisa likiendelea na hatua hii litaigawa kabisa  jumuia ya waanglikana na hiyo itakuwa na maana kwamba Kanisa la Uingereza limeshindwa kufanya kazi yake kama ambavyo limekuwa likifanya tangu zamani".

Naye Rv Sharon Ferguson, kutoka Chama cha Wasagaji na Mashoga wa Kikristo, alisema kuwa wanayakaribisha mabadiliko hayo. "Hizi ni habari njema kabisa," alisema. "Kama mtu katika mahusiano ya jinsia moja anayetekeleza mafundisho ya kanisa kuhusu maadili uhusiano wa kijinsia anaweza kuwa mtawa basi anatakiwa apewe nafasi ya kuwa askofu. Kwa hakika kwa asili marufuku hiyo ilikuwa ya kibaguzi."

Mwanamama huyo aliongeza kuwa uteuzi wa askofu shoga wa waziwazi ndio utakaomhakikishia kuwa kweli Kanisa limebadili sera yake. "Kusema kitu ni jambo zuri, kulitekeleza ni jambo jingine kabisa.'

Symon Hill, mwandishi wa Kikristo na mkurugenzi mshiriki wa taasisi ya Ekklesia, anasema kuwa Kanisa lilikuwa likifanya ubaguzi.

"Kwa bahati mbaya hili limetazamwa kama maendeleo lakini kwa kweli ni tangazo lingine la ubaguzi," alisema. "Linasema kuwa maaskofu wa kawaida wanaweza kuoa lakini maaskofu mashoga hawawezi kufanya hivyo. Useja ni zawadi kutoka kwa Mungu. Watu wengine wanapewa na wengine hawapendi. Sio chaguo bora la pili la utawa bora wa pili."

CHANZO: GAZETI LA THE INDEPENDENT
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment