![]() |
| Rais Yahya Jammeh wa Gambia |
Wagonjwa wa ukimwi watapatiwa matibabu ya mitishamba katika hospitali yenye vitanda 1,111 nchini Gambia, ambayo siku ya Jumanne Rais wa nchi hiyo alisema anapanga kuijenga licha ya wasiwasi wa wataalamu wa tiba kuwa matibabu hayo ni ya hatari.
Mwaka 2007 Rais Yahya Jammeh alisema kuwa amegundua tiba ya dawa ya mtishamba ya kuchemsha inayoweza kutibu UKIMWI, jambo lililoibua ghadhabu miongoni mwa wataalamu wa Kimagharibi waliodai kuwa rais huyo anawapa wagonjwa matumaini ya urongo.
“Baada ya mradi huu kuzaa matunda, tunakusudia kutibu wagonjwa 10,000 wa VVU/UKIMWI kwa kila miezi sita kupitia dawa za asili,” alisema Rais Jammeh katika hotuba yake ya mwaka mpya, na kuongeza kuwa hospitali hiyo yenye vitendo 1,111 itafunguliwa mwaka 2015.
Shirika la Afya Duniani (WHO) na Umoja wa Mataifa wamesema kuwa tiba ya Rais Jammed ya VVU/UKIMWI ni hatari sana kwa sababu wagonjwa wanatakiwa kuacha dawa za kupunguza makali ya Ukimwi (ARVs), na hivyo kukabiliwa na hatari ya mbinyo wa maradhi hayo.
Mwezi Oktoba, Jammeh alisema kuwa wagonjwa 68 wa VVU/UKIMWI waliokuwa wakipatiwa tiba hiyo ya mitishamba wamepona na kuruhusiwa, hilo likiwa kundi la saba tangu matibabu hayo yalipoanza miaka mitano iliyopita.
Viongozi wengine wa Kiafrika wamekabiliana na ukosoaji kwa kuitukuza uwezo wa tiba za mitishamba wa kupambana na UKIMWI.
Utawala wa Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Thabo Mbeki ilikashifiwa vikali kwa kukataa kwamba kulikuwa na uhusiano baina ya VVU na UKIMWI baada ya kushauri tiba kama vile mizizi ya viazi badala ya dawa zilizothibitishwa kimataifa.
Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, kiwango cha UKIMWI nchini Gambia ni cha chini ikilinganishwa na nchi nyingine za Kiafrika, ambayo ni asilimia 2 ya watu 1.8 ya watu walioambukizwa.
Jammeh aliingia madarakani katika mapinduzi ya kijeshi ambayo hayakumwaga damu mwaka 1994.
CHANZO: Reuters

0 comments:
Post a Comment