
Mwanaume mmoja katika jimbo la Bihar, nchini India alimchoma moto mkewe kwa sababu tu alisahau kuweka chumvi kwenye nyama.
Mama huyo mwenye majeraha makali alipelekwa katika hospitali ya eneo hilo kwa matibabu huko polisi wakiendelea kumsakama mwanaume huyo.
Tukio hilo la kikatili lilitokea katika kitongoji cha Alam Tota mashariki mwa wilaya ya Araria katika jimbo la Bihar Siku ya Alhamisi usiku lakini vyombo vya habari vikaripoti leo Jumamosi.
Polisi wanasema kuwa alhamisi usiku Nazarana Khatoon, mwenye umri wa miaka 25, alimtengea chakula mumewe baada ya kutoka kazini lakini alipoonja akakuta hakina ladha kana kwamba hakikuwekwa chumvi na kumfanya akasirike vibaya.
Mwanaume huyo aliyekuwa na hasira alichukua taa ya mafuta, akamwagia mkewe mafuta ya taa, akawasha kibiriti na kumchoma na kisha akamfungia chumbani.
Mtu mmoja alisikia mwanamke huyo akipiga kelele za kutaka msaada, akaenda kuwataarifu Polisi ambao walichelewa kufika hapo kutokana na kutokuwa na anuani kamili wakafanikiwa kumuokoa. Madaktari wanasema mama huyo ameungua kwa asilimia 40 na yuko katika hali mbaya.
“Polisi ndio walioweza, la sivyo angekufa kutokana na majeraha ya moto," msemaji wa Polisi katika kitongoji jicho, Shivdeep Waman Lande aliwaambia wanahabari. Alisema iliwachukua masaa matatu kumfikia muathirika kutokana na kutokuwa na anuwani kamili.
Lande alisema kuwa mwanaume aliyehusika alitoroka, lakini polisi wameanzisha msako mkali ili kumtia nguvuni. "Atakamatwa hivi karibuni," alisema Lande na kuongeza kuwa mwanamke huyo alipigwa vibaya sana kabla ya kuchomwa moto.
0 comments:
Post a Comment