![]() |
| BWANA HOSEA FOLORUNSHO AKIUFUKUA MWILI WA MWANAYE ALIYEMUUA KWA AJILI YA TAMBIKO |
Bwana Hosea Folorunsho, mkazi wa Jimbo la Kogi nchini Nigeria, amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mwanae kwa ajili ya tambiko. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishina wa Polisi, Bwana Mohammed Katsina, anasema mtuhumiwa, ambaye ni mganga wa tiba za jadi, alimzika mwanaye katika shimo nyuma ya nyumba yake.
Imeelezwa kuwa tarehe 31 mwezi wa Disemba mwaka 2012, bwana huyo alifanya unyama wa kumzika mwanaye kwa lengo la kafara au tambiko. Kwenye majira ya saa 5:55 Uisku kwenye kilele cha mwaka mpya, jamaa huyo alimchukua mwanaye huyo, Sanday Folorunsho na kumuua kinyama.
BwanaFolorunsho, mwenye umri wa miaka 48, ambaye ana mke na watoto watatu, alikamatwa na Polisi ambapo waliandamana naye mpaka eneo husika na kumlazimisha aufukue mwili wa kichanga huyo.
Baada ya mwili huo kufukuliwa, mtaalamu wa patholojia na kumfanyia uchunguzi ambao ulibaini kuumizwa vibaya sana baada ya kupigwa na kitu kizito.
CHANZO: NIGERIA INFO

0 comments:
Post a Comment