MAHABUSU aliyekuwa akishikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za wizi, amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya bukta aliyokuwa amevaa akiwa ndani ya mahabusu ya kituo cha polisi cha Wilaya ya Makete mkoani hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Fulgence Ngonyani alimtaja mahabusu huyo kuwa ni Chuki Semwa (21) mkazi wa Kijiji cha Isapilano.
Kwa mujibu wa Kamanda Ngonyani, mahabusu huyo alijinyonga juzi akiwa mahabusu wakati akisubiri kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za wizi zilizokuwa zikimkabili.
Ngonyani alisema, siku moja kabla ya kujinyonga, wananchi wa kijiji cha Isapulano walimfikisha mtuhumiwa huyo katika Kituo cha Polisi cha Makete, wakimtuhumu kuvunja nyumba mbili tofauti na kuiba Sh 18,000.
Alisema mtuhumiwa alikutwa na baadhi ya vitu vilivyodaiwa kuibwa katika nyumba hizo na kwamba wakati akisubiri kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili aliamua kujinyonga.
Alisema uchunguzi wa awali, umeonyesha kuwa mtuhumiwa huyo alijinyonga kwa kutumia kamba ya bukta aliyokuwa amevaa siku hiyo wakati akiwa mahabusu.
CHANZO: MTANZANIA
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment