Ajiua akihofia kuugua Ukimwi

MKAZI wa Kijiji cha Nyankorongo wilayani Chato mkoani Geita, Lameck Maraba (29) amejiua kwa kujikata koromeo baada ya kuhisi ana Ukimwi. Maraba ambaye amekuwa akiumwa kwa muda mrefu alishauriwa daktari apime afya yake.

Inadaiwa kuwa mwanakijiji huyo alifikia hatua hiyo usiku wa kuamkia juzi baada ya kushutushwa na ushauri wa daktari aliyemtaka kupima afya yake kubaini magonjwa yanayomkabili.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea wakati tayari zipo dawa za kuongeza maisha ambazo zimekuwa zikiwawezesha waathirika wa Ukimwi kuishi muda mrefu.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya, Pius Buchukundi alisema Maraba alifika hospitalini hapo Januari 17 akisumbuliwa na homa ya matumbo, malaria na upungufu wa damu na kutokana na hali hiyo alishauriwa kupima VVU .

Alisema baada ya kupata ushauri huo, hofu ilimjaa mwanakijiji huyo na hivyo kuamua kujikata koromero na kusababisha kifo chake.

Buchukundi ameshauri wagonjwa wanaokwenda kutibiwa hospitalini hapo wafuate ushauri unaotolewa na wauguzi kuepusha vifo visivyo vya lazima.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment