MAANDALIZI YA KOMBE LA DUNIA: MAKAHABA WA KIBRAZIL KUJIFUNZA KIINGEREZA BURE

MAKAHABA WA BRAZIL




Wakati nchi ya Brazil ikiandaa kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2014, makahaba katika mojapo ya miji mikubwa ya nchi hiyo hawako nyuma, wamejiunga na madarasa ya Kiingereza yatakayowawezesha kuwasiliana vizuri na wateja wa kigeni.

Kiasi cha makahaba 20 tayari wameshajiunga na kozi hiyo inayoandaliwa na Chama cha Makahaba katika mji wa Belo Horizonte, katika mkoa wa kusini mashariki ya nchi hiyo. Kiongozi wa kundi hilo, Cida Vieira, alisema kuwa anatarajia kwa uchache wanachama 300 kati ya 4,000 wa chama hicho watajiunga na madarasa hayo yatakayoanza mwezi wa Machi.

Aliongeza kuwa chama chao kinatafuta walimu wa kujitolea. “Sidhani kama tutatkuwa na shida ya kuwashawishi walimu wa lugha ya Kiingereza kuja kutoa huduma bure,” alisema kama alivyonukuliwa na shirika la habari la AP. “Tayari tuna wanasaikolojia na madaktari kadhaa wanaojitolea.”

"Itakuwa muhimu kwa mabinti watakaoweza kutumia Kiingereza wawajuze wateja wao kama wanatoza kiasi gani na kujua kile wanachokitaka," Vieira aliliambia shirika hilo, akaongeza kuwa chama chake pia kinafikiria kuweka madarasa yatakayofundisha lugha za Kifaransa na Kiitalia.

Hata hivyo, tangazo hilo limeibua moto miongoni mwa wenyeji, huku gazeti la Folha de Sao Paolo likichapisha maoni ya msomaji mmoja aliyeeleza kushangazwa na kuziita habari hizo kuwa “ajabu kubwa.”
 “Hii ni nchi inayotakiwa kuheshimiwa?… inayojifanya kuwa inapiga vita utalii wa ngono na unyonyaji mwingine wa ukoloni wa karene ya 18,’ alisema Nereu Augusto, akieleza kuwa nchi yake inaweza kuwa “ya ajabu” kweli kweli.

Mji wa Belo Horizonte unatarajia kuwa mwenyeji wa mechi tatu za Kombe la Mabara na michezo sita ya kombe la Dunia la mwaka 2014.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment