BALOZI WA HONDURAS AFUKUZWA KAZI KWA SABABU YA KARAMU YA VIDOSHO



Kufuatıa karamu ya ulevi na uasherati iliyohusisha makahaba na vidosho, balozi wa Honduras nchini Colombia amepoteza kazi yake. Nyaraka muhimu na nyeti zinaaminika kuibiwa baada ya wanawake ha ona wageni wengine kufanya wizi katika ubalozi huo mjini Bogota.

Wizi huo ulifanyika wakati watu wakiburudishwa na vidosho na makahaba. Tukio hilo lilikuwa baya sana kiasi kwamba kuna uchafu uliokutwa katika ofisi ya balozi.

Inadaiwa kuwa balozi Carlos Humberto Rodriguez hakuwepo wakati wa karamu hiyo iliyofanyikwa tarehe 20 Desemba.

Vyombo vya habari vya nchi hiyo, vinasema kuwa msaidizi wa balozi ndiye aliyeandaa ‘party’ hiyo iliyopelekea kompyuta na simu kuibwa. Ushahidi wa uchafu ulipatikana katika jengo hilo.

Siku iliyofuata, wafanyakazi walimkuta msaidizi huyo, Jorge Mendoza, akiwa amelala katika eneo la kufulia huku mfanyakazi mwingine raia wa Colombia akiwa amelala sehemu ya chini ya nyumba hiyo, linasema gazeti la El Heraldo. Gazeti hilo linadai kuwa marafiki wa  Mendoza na makahaba hao waliondoka mahali hapo wakiwa na kompyuta na simu kadhaa za mkononi. Kwa sasa polisi wanwasaka makahaba hao.

Inadaiwa kuwa kompyuta na simu hizo zilizoibiwa zina taarifa muhimu nan yeti kuhusu biashara ya madawa ya kulevya. Honduras ni kitovu muhimu cha biashara ya madawa ya kulevya ya Colombia.

CHANZO: RT
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment