KANISA KUU LA MAREKANI KUFUNGISHA NDOA ZA JINSIA MOJA



Kanisa kuu la Kitaifa la mjini Washington, mahali ambapo taifa hukusanyika kuomboleza misiba mbalimbali na kusherehekea uteuzi wa marais wapya, hivi karibuni litaanza kufungisha ndoa za jinsia moja.

Maafisa wa Kanisa wameliambia shirika la habari la The Associated Press kuwa kanisa hilo litakuwa la kwanza katika makanisa kufungisha ndoa za mashoga, wasagaji, na wapenzi wa jinsia moja. Kanisa litatangaza sera yake mpya siku ya Jumatano.

Kama kanisa maarufu zaidi na kubwa katika taifa, uamuzi huo utabeba ishara na athari kubwa. Kwa muda mrefu, kanisa hilo lenye umri wa miaka 106 limekuwa kituo cha kiroho kwa taifa hilo, likiwa mwenyeji wa ibada za uapishwaji wa marais mbalimbali kuanzia kwa Marais Ronald Reagan na Gerald Ford. Hutembelewa na maelfu ya watu.

Kuhusu uhalali wa ndoa za jinsia moja katika Wilaya ya Columbia na sasa Maryland, Rt. Rev. Mariann Edgar Budde, askofu wa kanisa la Washington, mwezi Desemba aliamua kuruhusu kutolewa kwa Sakramenti ya ndaoa ya Kikristo. Dayosisi hiyo inajumuisha wilaya hiyo na kaunti nne za Maryland. Dayosisi husika ina hiyari ya kuyafanyia kazi mabadiliko hayo. Na hivyo kila askofu katika Dayosisi husika anaweza kuamua kufungisha ndoa za jinsia moja au la.

Askofu Rev. Gary Hall, mkuu wa kanisa hilo, anasema kuwa kufungisha ndoa za jinsia moja ni fursa ya kuondosha vikwazo na kujenga jamii jumuishi "inayoakisi ulimwengu anuai wa Mungu."


"Ninesoma Biblia kwa umakini kama wafanyavyo watu wenye msimamo mkali," Hall aliiambia AP. "Usomaji wangu wa Biblia unaniongoza kutaka kufanya hivyo kwa sababu ninadhani muhimu ni kuwa na imani ya jamii ambayo Yesu angependa kuiona."

Kufungisha ndoa za jinsia moja ni jambo muhimu nje ya Kanisa, alisema Hall. Mjadala wa Kanisa kwa kiasi kikubwa umejikita kwenye suala hili na kuyapa makanisa husika hiar, alisema. Hatua hiyo pia inatoa fursa ya kuwa na nguvu katika taifa.

"Kanisa la umma katika mji mkuu wa nchi, kwa kusema kuwa tutazibariki ndoa za jinsia moja, kufungisha ndoa za jisnia moja, tunakuwa tumejaribu kuchukua hatua nyingine ya usawa wa mahusiano ya ndoa katika taifa na katika utamaduni," alisema Hall.

Hall ni kiongozi wa 10 wa kanisa hilo na amejishughulisha na huduma za kidni kwa zaidi ya miaka 35. Anasema kuwa alianza kufungisha ndoa za jinsia moja tangu mwaka 1990 alipokuwa akihudumu katika kanisa la All Saints Church la Pasadena, California.

Itachukua muda wa miezi sita mpaka mwaka mmoja kabla ndoa ya kwanza haijafungwa katika kanisa hilo kutokna na ratiba yake kujaa muda mwingi na kutokana na mahitaji ya awali ya ndoa hiyo. Kwa ujumla, wanandoa wanaohusika na kanisa hilo ndio watakaopata fursa kubwa. Viongozi wa kanisa hawajapokea maombi yoyote ya kufungisha ndoa kabla ya tangazo lao watakalolitoa siku ya Jumatano.

Wakati Hall akiwa hatarajii pingamizi lolote ndani ya Baraza Kuu la Kanisa, anasema kuwa mabadiliko hayo yanaweza kuibua ukosoaji kutoka nje. Linaweza kuwagawa baadhi, kama ilivyotokea wakati wa kuhubiri vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na suala la kuwaingiza wanawake katika nafasi za uaskofu, alisema Hall.

Kanisa la New York ni sehemu ya kanisa la Kianglikana lenye wafuasi milioni 77. Mwaka uliopita, Baraza la Maaskofu lilipitisha azimio namba 111-41 kuruhusu utoaji wa huduma ya kufungisha ndoa za jinsia moja.  Baadhi ya maaskofu wamelikimbia kutokana na kuwaingiza mashoga na wasagaji ndani ya kanisa hilo.

Kwa sasa ndoa za jinsia moja zimehalalishwa katika majimbo tisa na Washington, D.C. Wabunge katika majimbo ya Illinois na Rhode Island wanaandaa miswada itakayoruhusu ndoa hizo, na Mahakama Kuu imepanga kusikiliza kesi zinazohusu ndoa za  mashoga katika mwezi wa Machi.

Ndoa ya kwanza ya jinsia moja ilifungwa mwezi mmoja uliopita na kusababisha maandamano kutoka kwa wahafidhina. 

Hall, ambaye ni mkuu wa kanisa hilo, anasema kuwa kanisa lina historia ya muda mrefu katika misimamo inayohusu masuala ya umma. Lakini analiona sauala la ndoa kama suala la kibinadamu, sio la kisiasa.

"Kwa sisi kuweza kusema kuwa tunaikubali ndoa ya jinsia moja kama njia ya waamini kuishi maisha yao kama Wakristo katika wakati ambao vikwazo vingi dhidi ya usawa  kamili wa mashoga na wasagaji vinaondoka, nadhani ni kipindi muhimu sana."


CHANZO: www.dailystar.com
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment