WAPIGANAJI WA KIIRAQ WATISHIA KUYALENGA MASLAHI YA UTURUKI

Turkish Prime Minister Recep Tayyip Erdogan (file photo)
Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan



Kundi moja la wapiganaji wa Kiiraqi limetishia kuyalenga na kuyashambulia maslahi ya Uturuki katika kujibu kile kilicholalamikiwa kuwa ni "uingiliaji kati wa Uturuki uliovuka mipaka" katika masuala ya ndani ya Iraq.


“Tunapinga matamshi ya hivi karibuni ya Waziri Mkuu wa Uturuki [Recep Tayyip Erdogan] na kuyachukulia kuwa ni uingiliaji uliozidi wa mambo ya ndani ya Iraq,”' Asaib al-Haq alisema katika maelezo yaliyotolewa jana Alkhamisi. 

Mapema wiki hii, Erdogan aliishutumu serikali ya Iraqi kuwa ina mwenendo wa umadhehebu, akaonya kuwa Iraq inaweza kukumbwa na hali kama ya Syria. 

“Jaribio lolote la kuipasua Iraq [Umoja wa kitaifa] kwa kutengeneza umadhehebu na kueneza sumu ya mgawanyiko huyatia hasara maslahi ya wote, na atakayefanya hivyo hatokuwa salama,” kundi hilo lilisema. 

Uhusiano wa nchi hizi mbili uliharibika mwaka jana baada ya Uturuki kuelezea kumuunga mkono Makamu wa Rais wa Iraq anayetafutwa, Tariq al-Hashemi na kumpa hifadhi. Hashemi amehukumiwa adhabu ya kifo kwa madai ya kuhusika na vitendo vya kigaidi. 

Aidha, mashambulizi ya ndege za vita za Uturuki katika eneo la kaskazini mwa Iraq dhidi ya  ngome za Chama cha Wafanyakazi wa Kikurdistan (PKK) yamezikasirisha mamlaka za Iraq, wakiitaka Uturuki kuacha kuishambulia PKK kwenye ardhi ya Iraq.

Wapiganaji wa PKK wamekuwa wakipigana kujitenga kwa eneo la Wakurdi ndani ya Uturuki tangu miaka ya 1980. Mgogoro huu umewaacha makumi kwa maelfu ya watu wakiuawa. 

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment