
Wabunge wa Bunge la Somalia wameirejesha serikalini bajeti ya mwaka 2013 kwa minajili ya kufanyiwa marekebisho ya kimsingi. Taarifa kutoka Mogadishu zinasema kuwa, Wabunge hawakukinaishwa na matayarisho ya bajeti hiyo ya mwaka 2013 na kuitaka Wizara ya Fedha kuiangalia tena na kuifanyia marekebisho ya kimsingi kwa maslahi ya wananchi wa Somalia.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, bunge la nchi hiyo lilianza kuijadili bajeti hiyo tokea siku ya Jumatano baada ya kuwasilishwa bungeni na Mahmoud Hassan Suleiman Waziri wa Fedha wa nchi hiyo.
Duru hizo pia zimeeleza kuwa, bajeti ya Somalia katika mwaka 2013 itakuwa kiasi cha dola milioni 103 na laki tisa. Wizara ya Fedha imepewa muda wa mwezi mmoja wa kuifanyia marekebisho kabla ya kuirejesha tena bungeni kwa lengo la kujadiliwa na hatimaye kupitishwa na wabunge hao.
0 comments:
Post a Comment