Tarehe 17 ya mwezi wa Oktoba Ikulu ya Ufaransa ya Élysée ilitoa taarifa ya kuungama kwamba vikosi vya usalama vya nchi hiyo viliwakandamiza na kuwaua raia wa Algeria waliokuwa wakiandamana mjini Paris siku ya tarehe 17 Oktoba mwaka 1961. Sehemu moja ya taarifa hiyo imeeleza kama ninavyonukuu:" Tarehe 17 Oktoba mwaka 1961 Waalgeria waliokuwa wakiandamana kupigania uhuru wa nchi yao waliuawa kutokana na ukandamizaji wa umwagaji damu" mwisho wa kunukuu. Kwa mara ya kwanza Ikulu ya Élysée ilikiri kwa kutoa maelezo yafuatayo:" Jamhuri ya Ufaransa, baada ya kupita miaka 51 ya maafa haya inakiri kujiri kwake na inawakumbuka waliopoteza maisha yao katika tukio hilo".
Kwa mujibu wa takwimu mbalimbali watu 200 waliuawa, miongoni mwa Waalgeria wapatao elfu 30 waliokuwa wakiandamana mjini Paris kuitikia wito wa Harakati ya Taifa ya Ukombozi wa Algeria (FLN). Tangu mwaka jana hadi sasa, na katika minasaba tofauti na hasa wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais, Farncois Hollande aliwahi kutamka kwamba endapo atafanikiwa kuingia Ikulu atakuwa na mtazamo upya juu ya historia ya pamoja ya Algeria na Ufaransa. Mara moja Hollande alitembelea eneo la Mto Seine, mahali lilipotokea tukio la mauaji ya raia wa Algeria na kuweka shada la maua kama kumbukumbu kwa watu walipoteza roho zao na kisha akapaza sauti kwa kusema:" Ni lazima kukiri juu ya kile kilichotokea Oktoba 17 mwaka 1961. Lilitokea tukio la maafa, nami ninakiri kwamba ni kweli lilitokea na hata nilishawahi kusaini barua chungu nzima za malalamiko kuhusiana na suala hili. Na kwa kuamua leo kufika mahali hapa ninakiri juu ya kutokea jinai hii", mwisho wa kumnukuu.
Hata hivyo licha ya kuungama juu ya kutokea jinai ya mwaka 1961, Ikulu ya Élysée haikuwa tayari kuomba radhi kwa jinai hiyo wala kuonyesha masikitiko kwa Waalegria ambao ni manusura wa mauaji hayo wanaoishi hivi sasa nchini Ufaransa. Pamoja na hayo kwa mtazamo wa weledi wengi wa mambo, kukiri Ikulu ya Élysée kuwa mauaji ya mwaka 1961 ya raia wa Algeria nchini Ufaransa yalikuwa tukio la jinai ni hatua ya kutaka kuwahadaa watu ili kunufaika na suala hilo kisiasa na kipropaganda na kuzipotosha fikra za waliowengi. Kwani kama kweli viongozi wa Ufaransa wanahisi aibu na fedheha kutokana na jinai zilizofanywa na waliowatangulia na wanataka kuungama kwa jinai walizotenda, basi wangepasa kuyapa kipaumbele na umuhimu zaidi matukio ya mauaji ya mamia ya maelfu ya Waalgeria waliouawa katika kipindi cha miaka 132 ya kukoloniwa nchi yao na Ufaransa. Kwani jinai iliyotendwa na serikali ya Ufaransa Oktoba 17 mwaka 1961 mjini Paris ikilinganishwa na mauaji ya zaidi ya Waalgeria milioni moja waliouliwa wakati wa ukoloni na hasa katika kipindi cha mapambano ya kupigania uhuru cha kati ya mwaka 1954 hadi 1962 ni sawa na kulinganisha jinai yenye ukubwa wa mlima na ile ya kichuguu.
Kwa muda wa miaka 132, yaani kuanzia mwaka 1830 hadi 1962, Algeria ilikuwa chini ya ukoloni wa Ufaransa. Katika kipindi hicho na hasa wakati yalipopamba moto mapambano ya wananchi wa Algeria dhidi ya ukoloni, Wafaransa walifanya jinai za kinyama na za kutisha. Wakati wa mapinduzi ya uhuru wa Algeria nchi hiyo ilikuwa na watu wapatao milioni tisa ambapo karibu milioni moja kati ya hao waliuliwa kwa halaiki na jeshi la Ufaransa.
Mbinu nyingi za utesaji ambazo zilikuja kuzoeleka na kutumika baadaye ulimwenguni zilibuniwa na kuanza kutumiwa na wakoloni wa Kifaransa nchini Algeria. Jinai zilizofanywa na Ufaransa nchini Algeria zilikuwa kubwa na za kutisha kiasi kwamba zililalamikiwa na kupigiwa makelele ya upinzani duniani mpaka ndani ya Ufaransa kwenyewe, na hivyo ili kujivua na dhima ya jinai hizo kiongozi wa nchi hiyo Jenerali Charles de Gaulle akaamua kuwaita wanajeshi na maafisa wake wa kisiasa nchini Algeria kuwa ni "waasi". Kwa kweli uasi ilikuwa sifa waliyokuwa nayo askari wa Ufaransa, na si Algeria pekee walikofanya mauaji ya kimbari bali waliingilia na kukandamiza harakati nyingi za wananchi katika nchi za Chad, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Gabon, Ivory Coast na Kongo. Nukta ya kushangaza ni kwamba kizazi cha sasa cha viongozi wa Ufaransa sio tu hakijaonyesha majuto yoyote kutokana na jinai hizo bali ni kinyume chake, kwani mnamo mwezi Februari mwaka 2005 bunge la taifa la nchi hiyo lilipasisha muswada unaosifu na kupongeza kile kilichotajwa kuwa ni "mchango chanya" wa Ufaransa katika makoloni yake na muswada huo ukaingizwa kwenye vitabu vya masomo vya shule za nchi hiyo. Katika kifungu cha kwanza cha sheria hiyo imeelezwa hivi:" Taifa linadhihirisha upeo wa shukurani kwa wanawake na wanaume ambao walifanya juhudi za kutekeleza malengo ya nchi hii katika maeneo ya zamani ya Ufaransa ya mamlaka ya Ufaransa katika nchi za Algeria, Morocco, Tunisia, India na China na katika ardhi nyenginezo ambazo kabla ya hapo zilikuwa zikijulikana kuwa sehemu ya ardhi ya Ufaransa". Na katika kifungu cha 4 cha sheria ya kuunga mkono jinai zilizofanywa na Ufaransa katika makoloni yake imeelezwa hivi:"Katika mitalaa ya vyuo vikuu inatakiwa ipewe umuhimu maalumu historia ya uwepo wa Ufaransa katika ardhi za nje ya mipaka ya bahari na hasa Afrika Kaskazini." Mwisho wa kunukuu. Ukweli ni kwamba serikali ya Ufaransa sio tu haioni aibu kwa mauaji ya kutisha iliyofanya katika kipindi cha miaka minane ya Waalgeria milioni moja bali inaona fahari na kujivunia jambo hilo.
Baada ya kupasishwa sheria hiyo hakuna chama chochote kilichoingia madarakani nchini Ufaransa kilichopinga, na ndio kusema kuwa kimya chao ni ishara ya kuridhia mauaji hayo ya halaiki ya mamia ya maelfu ya watu wasio na hatia ambao waliuawa kinyama kwa sababu tu ya kupigania uhuru na kujitawala nchi yao. Ukubwa wa jinai zilizofanywa na Ufaransa katika ardhi ya Algeria hauwezi kufananishwa na simulizi za ngano zinazotolewa za mauaji ya Mayahudi katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Katika simulizi za Mayahudi wa Kizayuni na baadhi ya waandishi wa Magharibi, zinazungumziwa sana habari za matanuri ya gesi yaliyotumiwa na Manazi wa Ujerumani katikaa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia katika mauaji ya Mayahudi. Na hii ni katika hali ambayo wanajeshi wa Ufaransa walitumia sana mbinu hiyo ya matanuri ya gesi kuwaua kwa halaiki wanamapambano wapigania uhuru wa Algeria.
Muhammad al Kurso, mwanahistoria wa Algeria anasema kuhusiana na mauaji ya wapigania uhuru wa Algeria yaliyofanywa na Wafaransa ya kwamba, kulingana na nyaraka za kutisha za historia, jeshi la Ufaransa lilitumia mbinu ya kuua watu kwa halaiki kwa kutumia gesi ya sumu katika kipindi cha karne moja kabla ya Manazi wa Ujerumani. Al Kurso anabainisha jinsi wanajeshi wa Ufaransa walivyokuwa wakiweka uzio wa ukuta kuzunguka mapango yaliyokuwa yakitumiwa na wananchi wa Algeria kwa ajili ya kujificha na kisha kujaza moshi wa moto na gesi ya sumu ndani ya mapango hayo. Kwa hakika huo ni ukweli wa matukio ya historia ambayo yanazidi kuielemea serikali ya Ufaransa inayojaribu kuhadaa fikra za waliowengi. La ajabu ni kwamba ni mwiko nchini Ufaransa kukosoa kwa namna yoyote ile madai ya Wazayuni kuhusiana na kuuawa Mayahudi katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, na anayejusuru kufanya hivyo huhukumiwa kifungo jela na kupigwa faini pia. Lakini jinai zisizoweza kufikirika zilizofanywa na askari wa Ufaransa za kuwaua raia milioni moja wa Algeria zinatajwa kama kazi nzuri na mchango chanya uliotolewa na Ufaransa katika enzi zake za ukoloni. Hiki wapenzi wasikilizaji ndio kioja cha kutia uchungu cha dunia yetu ya leo. Wale wanaojidai kuwa watetezi wa demokrasia na haki za binadamu duniani hawako tayari hata kuonyesha majuto kwa jinai za kinyama walizofanya na kuyaomba radhi mataifa waliyoyakoloni huko nyuma, lakini kwa kutumia kisingizio cha kutetea haki za binadamu na demokrasia wanajipa idhini na mamlaka ya kuingilia masuala ya ndani ya mataifa mengine katika kila pembe ya dunia. Si Ufaransa peke yake bali madola yote ya kikoloni ya Magharibi kuanzia Marekani, Uingereza, Italia, Ubelgiji, Uholanzi, Uhispania na hata Ureno hayako tayari kuomba radhi kwa mauaji yaliyofanya ya mamilioni ya watu, mbali na mamilioni ya wengine waliowafanya watumwa. Madola ambayo yanaona fahari kwa rekodi zao chafu na mbaya za huko nyuma leo hii yamegeuka kuwa wasamaria wema wa jamii ya wanadamu.
Pamoja na hayo ungamo la Francois Hollande kwamba mauaji ya mwaka 1961 ya Waalgeria 200 mjini Paris yalikuwa tendo la jinai halikutoa mguso wala kupata radiamali ya maana ndani ya Ufaransa kwenyewe. Na hii inaonyesha kuwa kila mtu anajua kwamba matamshi hayo yametolewa kwa lengo la kuwahadaa watu. Ikiwa Rais wa Ufaransa anaamini kwa dhati kwamba mauaji hayo yalikuwa tendo la jinai inampasa atangaze pia msimamo wake kuhusiana na mauaji ya raia milioni moja wa Algeria waliouliwa na askari wa Ufaransa wakati walipokuwa wakipigania uhuru wa nchi yao…/
CHANZO: IRIB

0 comments:
Post a Comment