JULIAN ASSANGE KUCHAPISHA MAMILIONI ZAIDI YA NYARAKA ZA SIRI

MUASISI WA MTANDAO WA WIKILEAKS, JULIAN ASSANGE



MUASISI wa mtandao wa WikiLeaks, Julian Assange, amesema atatoa zaidi ya nyaraka nyingine milioni moja mwaka ujao ambazo "zitaigusa kila nchi duniani".

Mwanaharakati huyo hujitokeza kwa nadra hadharani chini ya hifadhi ya ubalozi wa Ecuador mjini London, alikokimbilia miezi sita iliyopita kukwepa kukamatwa na kupelekwa Sweden kwa madai ya uhalifu wa udhalilishaji wa kijinsia.

Akihutubia umati wa mashabiki wake 200 na vyombo vya habari vya kimataifa, alisema: "WikiLeaks ina zaidi ya nyaraka milioni moja ambazo ziko tayari kutolewa hadharani. Nyaraka ambazo zitaigusa kila nchi duniani. Kila nchi duniani. Na nchini Australia seneta ambaye hakuchaguliwa atabadilishwa na yule aliyechaguliwa."

Assange alikataa kuacha kujificha akisema kuwa alimehifadhiwa katika ubalozi huo kwa kuhofia uchunguzi na upelelezi unaofanywa na Marekani kuhusu harakati zake. 

'Kazi Itaendelea'

"kazi yangu haitasimama, lakini wakati uchunguzi huu usio sahihi ukiendelea na kwa ikiwa serikali ya Australia haitaitetea kazi ya habari na machapisho ya WikiLeaks nitaendelea kuwa hapa," alisema Assange.
"Lakini, milango iko wazi na imekuwa wazi kwa kila anayetaka kuzungumza na mimi. Kama ilivyo kwa upande wenu, sijashitakiwa kwa uhalifu wowote," alisema.

Aidha, alitaja orodha ya watu waliowekwa magerezani, kama vile mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka Bahraini Nabeel Rajab na mdukuzi wa Anonymous Jeremy Hammond.

Muaustralia huyo mwenye umri wa miaka 41 alimsifu askari wa Kimarekani, Bradley Manning, aliyewekwa kizuizini kwa madai ya kuwa ndiye aliyekuwa akiipatia WikiLeaks taarifa za siri zilizoikasirisha serikali ya Marekani. 

"Bradley Manning, ambaye wiki hii ametimiza umri wa miaka 25, ni kijana ambaye ameitunza heshima yake baadaya kutumia zaidi ya asilimia 10 ya umri wake akiwa gerezani bila kufunguliwa mashitaka yoyote, wakati mwingine oni, akiwa uchi na bila miwani yake," alisema. 

Assange anachunguzwa na maafisa wa Marekani kwa kuvujisha nyaraka za siri na pia anatakiwa kwa madai ya tuhuma za udhalilishaji wa kijinsia anaodaiwa kuufanya wakati alipoitembelea Sweden mwaka 2010.

CHANZO: ALJAZEERA.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment