28 WAUAWA KATIKA MAPIGANO YA KIKABILA NCHINI KENYA
Kwa uchache watu 28 wanaripotiwa kuuawa katika eneo la Tana River nchini Kenya baada ya watu wasiojulikana kufanya mashambulio katika kijiji cha Kipau alfajiri ya leo. Polisi ya Kenya imesema kuwa, watu 28 wamethibitishwa kuwa wamepoteza maisha na kwamba, kuna uwezekano wa kuongezeka idadi hiyo. Baadhi ya mashuhuda wanasema, kungali kuna maiti jirani na vichaka vya eneo hilo. Eneo la Tana River nchini Kenya lilishuhudia machafuko makubwa kabisa mwezi Agosti na Septemba mwaka huu ambapo watu zaidi ya mia moja waliuawa wakiwemo maafisa wa polisi. Makabila ya Pokomo na Orma ya eneo hilo la Kenya yamekuwa yakipigania ardhi ya malisho kwa muda mrefu na katika miezi ya Agosti na Septemba mvutano huo wa ardhi uligeuka na kuwa mapigano ya silaha. Wakati huo huo imeelezwa kuwa, idadi ya watu waliojiandikisha nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki katika uchaguzi ujao wa Machi mwakani ni milioni 14 na laki tatu. Zoezi la uandikishaji wapiga kura lilianza Novemba 19 mwaka huu na kuendelea hadi Alkhamisi ya jana.
SOURCE; IRIB

0 comments:
Post a Comment