Bunge la marekani limepitisha "sheria ya ulinzi" inayojumuisha vikwazo vipya dhidi ya Iran, dola nyingine zipatazo milioni 500 kwa ajili ya mfumo wa makombora wa utawala wa Israeli na kitita kingine cha fedha zinazokadiriwa kufikia dola bilioni 89 kwa ajili ya vita vya Afghanistan.
Aidha, hatua hizo zinalenga pia kuiwekea vikwazo mitandao ya habari ya Iran.
Wabunge wa marekani wameripotiwa kupitisha kilekinachoitwa kuwa ni sheria ya ulinzi, ambayo imeidhinisha kiasi cha dola milioni 480 kwa ajili ya mfumo wamakombora wa utawala wa Israeli na kupitishwa kwa kura 315 huku kura 107 zikiukataa muswada huo.
Aidha, muswada huo umetenga kiasi cha dola bilioni 88.5 kwa ajili ya harakazi za vita vinavyoongozwa na Marekani nchini Afghanistan, licha ya utawala wa Obama kutangaza mipango ya kuyaondoa majeshi yake katika taifa hilo la Asia.
Muswada huo pia umetenga dola bilioni 17 kwa ajili ya mpango wa Nyuklia wa Marekani.
Sheria hiyo sasa inasubiriwa kupitishwa na Baraza la Seneti kabla ya kusainiwa na Rais Barack Obama na kuwa sheria kamili.
Hata hivyo, Ikulu ya marekani, imetishia kutumia kura ya turufu, kulazimisha sheria hiyo kurudi bungeni kupitiwa na kupigiwa kura upya.
CHANZO: MFB/AZ

0 comments:
Post a Comment