WAHAMIAJI 55 WAHOFIWA KUFA MAJI NJE YA PWANI YA SOMALIA



Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa watu wasiopungua 55 wanahofiwa kuwa wamefariki dunia baada ya boti waliyokuwamo kuzama nje ya pwani ya Somalia.

Taarifa iliyotolewa na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa imesema maiti za watu 23 zimeopolewa majini na kwamba abiria wengine 32 wa boti hiyo wanadhaniwa kuwa wameghariki.

Boti hiyo ambayo inaaminika kuwa ilikuwa na raia wa Somalia na Ethiopia, ilikuwa njiani kutoka bandari ya kaskazini mwa Somalia ya Bosaso ikielekea Yemen. Watu 95 wameghariki na kufa maji mwaka huu pekee katika maji ya kati ya Somalia na Yemen.

Mwakilishi wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa nchini Somalia Bruno Geddo amesema kuwa ajali hiyo inaonesha hatari wanazokumbana nazo Wasomali wanaokimbia machafuko na ghasia nchini kwao.

SOURCE: IRIB
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment