NA HAMED MAZROUY
Makamo wa kwanza wa rais wa Zanzibar Maalim seif sharif hamad amesema kuwa Zanzibar inahitaji kujipanga zaidi ili iweze kulinda mafanikio yaliyopatikana kutokana na mradi wa kutokomeza malaria zanzinbar,amesema kua mafanik

io yalopatikana ndani ya nchi ya zanzibar yameiletea sifa kubwa sana nchi yetu mpaka kupelekea kuigwa na nchi nyengine duniani.
Maalim seif ameyasema hayo huko katika kitengo cha kudhibiti malaria zanzibnar kilichopo mwana kwerekwe mjini unguja wakati akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake yakutembelea taasisi zote zilizo chini ya wizara ya afya na ustawin wa jamii nkwa upande wa unguja,pia amesema mafanikio hayo yananpaswa kulindwa na kuhakikisha kuwa lengo la zanzibar bila ya kuwa na malaria linawezekana.
Kwa upande wake msimamizi meneja wa kitengo cha malaria zanzibar Bw,Mwinyi Msellem amesema kuwa zanzibar kwa sasa tayari imepata mafanikio ya kuweza kupambana na malaria katika kipindi cha miaka kumi illiopita ambapo kwa sasa maradhi hayo yapo chini kwa asilimia mmoja kutoka asilimia 45 mwaka 2001.
Kufuatia mwendelezo wa ziara hio maalim seif akiwa katika bohari kuu ya madawa zanzibar huko maruhubi makamo wa kwanza wa rais amesema ukweli nikuwa amefarijika kutokana na mfumo wa kisasa unaotumiwa wa uhifadhiji na utowaji dawa pamoja na usambazwaji wake katika vituo vya afya vilivyopo unguja na pemba.
Aidha kwa upande wake mfamasia mkuu wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar DR Habibi Ali Sharif amesema kuwa dawa zinaweza kuhifadhiwa katika bohari hio kwa kipindi cha miezi sita na kwa sasa wamekuwa tayari wakipokea mfumo wa maombi kwa vituo vya afya kwa ajili ya usambazwaji dawa.
Na huko katika bodi ya chakula,dawa na vipodozi,maalim seif amewataka wananchi za zanzibar kutoa ushirikiano kwa bodi hio ili iweze kufanya kazi zake vizuri ambazo zinalengo la kutunza afya kwa jamii ya watu wa zanizibar,aidha ziara hio pia imewashirikisha watendaji nwakuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii wakiwemo waziri wa wizara hio Mh Juma Duni Haji na katibu mkuu Dr Mohammed Saleh Jidawi.

0 comments:
Post a Comment