KESI DHIDI YA WAZIRI MKUU KUUNGURUMA


Kesi dhidi ya waziri mkuu wa mwisho wa Muammar Gaddafi,   bwana al-Baghdadi al-Mahmoudi, imepangwa kusikilizwa leo mjini Tripoli, Libya.

"Al-Baghdadi al-Mahmoudi atatokea kesho (leo) kwenye tukio la kesi ya kwanza dhidi yake," alieleza msemaji wa mwendesha mashtaka wa serikali, Taha Baara, akiongeza kuwa waziri mkuu huyo wa zamani anakabiliwa na mashtaka ya "vitendo vinavyohatarisha usalama wa taifa."

Mnamo Septemba 2011, Mahmoudi alikimbilia Tunisia kufuatia kupinduliwa kwa Gaddafi, ambaye aliuawa Oktoba 20 mwaka jana.

Mnamo Juni 24, 2012, alirejeshwa Tripoli baada ya kushikiliwa kwa miezi kadhaa nchini Tunisia. 


Waandishi wa habari walipotembelea gereza alililofungwa, aliwaambia: "Niko tayari kushitakiwa na wananchi wa Libya. Ninajiamini na pia nina uhakika kuwa sina makosa."

Mahmoudi alifanya kazi kama waziri mkuu tangu 2006 mpaka saa za mwisho za utawala wa Gaddafi mwaka 2011 na alikuwa mtiifu kwake mpaka dakika ya mwisho.


Kabla ya hapo, alishika nafasi mbalimbali serikalini, ikiwa ni pamoja na waziri wa afya 1992 mpaka  1997, waziri wa rasilimali watu na waziri wa miundombinu.

Mwezi Februari 2011 uliibuka uasi uliomuandosha Gaddafi madarakani Agosti 2011. Aliitawala nchi hiyo kwa zaidi ya miongo minne.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment